25 September 2013

PUSH MOBILE KUTOA GARI KWA MSHINDI WA FIESTA



Na Mwandishi Wetu
   Kampuni ya Push Mobile Media, itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz kwa mshindi wa promosheni ya tamasha la Serengeti Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza Ijumaa hii

    Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema watatoa gari aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika tamasha hilo kwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 na kuingia katika bahati nasibu hiyo.
Rodney alisema mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda fedha taslimu sh. 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta anaweza kushinda pikipiki.Mshindi wa Mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza wa gari alikuwa Abdallah Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha la Fiesta la Kigoma.
  "Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh. milioni 80 ili kufanikisha jambo hili ambapo magari aina ya Vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa nguvu zote," alisema Rodney. Wakati huo huo, mkazi wa Shinyanga, Rose Mahenda amafanikiwa kushinda pikipiki baada ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo.

No comments:

Post a Comment