Na Penina Malundo
Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi,amesema Serikali itahakikisha wahamiaji haramu
hawarudi nchini bila kufuata taratibu za kisheria zinazostahili kufuatwa. Dkt. Nchimbi aliyasema hayo Dar es Salam
jana wakatiakizungumza na waandishi wahabari na kutoa matokeo ya awali juu ya
utekelezaji Operesheni Kimbunga iliyolenga kuwaondoa wahamiaji haramu nchini
Alisema kupitia operesheni hiyo awamu ya
kwanza, wahamiaji haramu 12,604 wamerejeshwa katika nchi zao kutokana na agizo
la kiongozi wa nchi, Rais Jakaya Kikwete. "Kati ya wahamiaji hawa,Wanyarwanda ni 3,448,
Warundi 6,125, Waganda 2,496, Wakongo 589, Wasomalia 44, raia wa Yemeni mmoja
na India mmoja," alisema Dkt. Nchimbi na kuongeza;"Ni vyema wahamiaji haramu wakafuata
utaratibu wa kisheria,hata Watanzania wanaokwenda nchi nyingine nao wanapaswa
kufuata utaratibu na si vinginevyo,"alisema.
Alitoa
wito kwa Watanzania,kuacha utamaduni wa kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji
haramu jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao na nchi kwa ujumla. Alisema Watanzania
wanapaswa kuwa macho na wageni wanaoingia nchini kutoka nchi nyingine bila
kufuata taratibu za kuishi nchini kwani wengi wao wanauwezo wakufanya uhalifu hasa katika kipindi hiki cha usalama wa dunia
kuwa hatarini.
Aliongeza kuwa, katika operesheni hiyo
watuhumiwa 212 wa unyang'anyi wa kutumia silaha walikamatwa pamoja na mabomu 10
ya kutupwa kwa mkono, silaha 61, risasi 662 na mitambo miwili ya kutengeza
silaha aina ya magobori
No comments:
Post a Comment