Na Derick Milton, Simiyu
SHIRIKA la World Vision Tanzania limekabidhi mradi mkubwa
wa maendeleo kwa wananchi wa Kata za Nkoma na Mwalushu wilayani Itilima mkoani
Simiyu uliodumu kwa miaka 16 ambao umenufaisha wananchi 49,608.
Mr a d i h u o amb a o umekabidhiwa mwishoni mwa wiki kwa wananchi
ukiwa chini ya Halmashauri ya wilaya hiyo ulianzishwa mwaka 1998 ukiwa na lengo
la kuongeza ustawi kwa watu maskini hasa ustawi wa watoto ukiwa chini ya
shirika hilo kwa ufadhili wa watu wa nchini Newzeland.
Akitoa ufafanuzi juu mafanikio ya mradi huo tangu kuanzishwa kwake
hadi kumalizika Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania, Dkt. Kasilima
Yosh alisema kuwa mradi huo ulikuwa na lengo kuu moja kuleta ustawi kwa kila
mtoto.
Al i s ema mr a d i wa m a e n d e l e o N k o m a ulianzishwa
mwaka 1998 ambapo hadi kufikia mwisho wake umeweza kuleta maendeleo kwa
wananchi katika nyanja za kiuchumi, kiafya, kijamii, kiulinzi, pamoja na
kimaamuzi na haki zao kwa ujumla.
Alisema katika idadi hiyo ya wananchi walionufaika na mradi huo
wanawake ni 13,273, huku wanaume wakiwa 14,335, watoto wakiwa jumla yao 22,956, wa v u l a n
a 1 0 , 9 5 5 n a wasichana wakiwa 12,001.
Alisema katika mafanikio ya mradi huo kwa upande wa sekta ya
kilimo na uhakika wa chakula shirika hilo limefanikiwa kuunda vikundi 120 vya
wakulima wanaotumia njia nbora za kilimo, matumizi ya mbolea, pamoja na
uzalishaji wa mazao umeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Aliongeza wakulima wanaotumia njia bora za kilimo wameongezeka
kutoka asilimia 7 mwaka 1998 hadi kufikia asilimia 47 kwa mwaka huu, ambapo
katika sekta ya afya jumla ya wahudumu wa afya 32 wamepewa mafunzo ya kuhudumia
jamii katika huduma za afya.
Alibainisha magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na maji nayo
yamepungua kutoka asilimia 87 hadi kufikia asilimia 24 kwa mwaka huu, ikiwa
pamoja na kupungua kwa utapiamlo mkali na wa kati kwa watoto chini ya miaka 5
kutoka 42 miaka 0.6 na ule wa kati kutoka asilimia 25 hadi kufikia 0.
Aidha alisema katika upande wa elimu katika mradi huo shirika
limefanikiwa kujenga jumla ya madarasa 55, kwa kushirikiana na Serikali
kukarabati madarasa 9, nyumba 2 za walimu, ofisi 16 za walimu nazo zimejengwa
na mradi, vitabu 3,850 vimetolewa kwa shule 11, pamoja na kutoa madawati 1,126
kwa shule 11.
Akipokea mradi huo Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Paschal Mabiti ambaye pia alikuwa mgeni rasmi alilipongeza shirika hilo kwa kazi hiyo kubwa
ikiwa pamoja na kuwataka viongozi wa halmashauri kuhakikisha mradi unakuwa
endelevu pamoja na kutunzwa.
No comments:
Post a Comment