Na Lilian Justice, Mvomero
WASOMI wa Chuo Kikuu
Mz umb e k i l i c h o p o wilayani Mvomero mkoani Morogoro wamesema kuwa ni
vyema Rais akaondolewa kinga ya kushtakiwa pindi anapotuhumiwa kwa makosa ya
rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma
. Hayo yalibainishwa jana na wanajumuiya hao kwa nyakati wakati
wakijadili rasimu ya katiba kwa mwaka 2013 ambapo Mkurugenzi wa masomo ya
shahada ya kwanza chuoni hapo, Prof George Shumbusho alisema ni vyema rais
akapewa kinga kwa masuala ya kawaida na si masuala ya rushwa, ufisadi na
matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
A i d h a w a s o m i h a o wamependekeza Katiba Mpya, k u r u h u
s u u a n z i s hwa j i wa Mahakama ya Rushwa kama ilivyo kwa Mahakama za
Ardhi, biashara na nyingine, ili kutoa nafasi kwa suala hilo kushughulikiwa kwa
mapana zaidi tofauti na hivi sasa.
Pia mwanafunzi wa chuo hicho, Ester Safari alisema kitendo cha
kuwapeleka watuhumiwa wa rushwa katika mahakama za kawaida, kumesababisha
mrundikano wa mashauri mengi kwa waendesha mashtaka na mahakimu.
Aidha walisema kuwa kesi hizo zimeonekana kukosa nafasi ya kutosha
badala yake kuonekana ni masuala ya kisiasa zaidi, hivyo kupendekeza rushwa
kuwa na mahakama yake itakayokuwa na waendesha mashtaka wake ili kutilia mkazo
vita dhidi ya rushwa.
Kwa upande wake Mhadhiri msaidizi Kitivo cha Sheria chuoni hapo,
Dkt. Eliuther Mushi pamoja na mambo mengine, amependekeza suala la jukumu la
usafi wa mazingira kwa kila mtu iwe ni wajibu wa kikatiba ili kumfanya
Mtanzania kuwajibika na usafi katika maeneo yake badala ya kusubiri kazi hiyo
kufanywa na halmashauri.
Aidha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Taaluma, Prof.
Josephat Itika, ameshauri suala la uzalendo kupewa kipaumbele kikatiba na suala
la kujitegemea likatambulika kikatiba, ili kijana tangu utoto wake ajue suala
hilo ni la lazima.
Aidha wachangiaji wengine, Mhadhiri msaidizi wa chuo hicho,
Innocent Mgeta, mwanafunzi, Charles Ntwale na mwezeshaji, Benjamini Jonas,
wamependekeza katiba ijayo yenye Serikali tatu iwe na Rais mmoja wa muungano na
kwa upande wa nchi washirika yaani Zanzibar na Tanganyika kuwe na mawaziri
wakuu ili kupunguza gharama zisizokuwa na lazima.
Hata hivyo wamelitaka suala la ardhi na maziwa kuwekwa wazi katika
katiba ili yatambulike wazi, tofauti na sasa jambo linapelekea wananchi
kushindwa kushirikishwa na kunufaika na rasilimali hizo.
No comments:
Post a Comment