30 September 2013

WASHIRIKI WA EBSS KUJULIKANA WIKI HII Na Mwandishi Wetu
  Washibiki wawili waliofanikiwa kuingia fainali za mashindano ya kuimba la Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa njia ya simu watajulikana wiki hii, baada ya kuwashinda wenzao zaidi ya 3,000 walioshiriki kupitia simu za mkononi.

Washiriki hao wawili wataungana na wenzao 10, ambao jana walifanikiwa kuingia hatua hiyo kati ya 15 waliokuwa wamebaki.Mashabiki wengi wa mashindano hayo wanawasubiria kwa hamu washiriki hao hasa baada ya mshiriki kwa njia ya simu wa mwaka jana, Menina Atick, kufanya vizuri.Hadi sasa wamebaki washiriki 10 ambao ni Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya, First Godfrey, Francis Flavian, Furaha Charles, Furaha Mkwama, Joshua Kahoza, Maina Thadei na Mandela Nicolus.
  Washiriki waliotoka jana ni Fatma Omary mshiriki kutokea Dar es Salaam, Joseph Kura mshiriki kutoka Arusha na Catherine Mtange wa Dar es Salaam.Wengine walioaga ni Joseph Meteka na Kennedy Gedeon ambapo washiriki waliotolewa kwenye 'danger zone 'na kurudia katika kundi la washiriki wa kawaida ni Furaha Mkwama na Mandela Nikolas.No comments:

Post a Comment