30 September 2013

LULU AWATAKA WAZAZI KUWAPA WATOTO FURSANa Mwandishi Wetu, Mwanza
  Mamlaka  ya wakazi wa jiji la Mwanza juzi wamejitokeza katika semina ya fursa inayokwenda sambamba na Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika katika Mikoa ya Tanzania Bara ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa Gold Crest jiini hapa
.  Katika tukio msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' alikuwa kivutio kikubwa kutokana na watu wengi kuwa na hamu ya kumuona na kutaka kujua ataongelea jambo gani au atachangia mada ipi.
Akizungumzia jinsi kipaji chake kilivyopatikana tangu akiwa mdogo msanii huyo alisema alikipata baada ya kukutana na muigizaji wa kundi la Kaole Mahfidh Awadh 'Dkt. Cheni' ambaye alikuwa akipita mara kwa mara mtaani kwao, wakati huo alikuwa na umri wa miaka mitano.
"Nilipokutana naye nikamtolea mfano wa kuigiza kama ninalia, akashangaa na kuniambia kuwa unaweza, mwambie mama yako akulete Kaole, mama iliona fursa na haikumchukua muda mrefu kunipeleka Kaole kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba naweza kuigiza na kuwa msanii mkubwa, pia nilimsumbua sana," alisema Lulu.
Tofauti na watu wengi walivyokuwa wakifikiria nini msanii huyo ataongelea, Lulu pia alitoa mifano mingine ya jinsi wazazi wanavyo wanyima fursa watoto wao ikiwemo ya mtoto akiwa anaimba.

No comments:

Post a Comment