Na David John
WANANCHI wa Kijiji cha Kidomole,
Kitongoji cha Vihagatta Kata ya F u k a y o s i wi l a y a n i Ba g amo y o mk
o a n i Pwa n i wamevamia mashamba yaliyopo katika kijiji hicho na kugawana
maeneo kwa madai kuwa viongozi wa halmashauri ya mji huo wanayauza kinyemela
kwa watu wasiojulikana
.Akizungumzia na Majira mapema
wiki hii, Mwenyekiti wa Kamati maalumu ya wananchi hao, Salum Mubalule alisema
wamechoshwa na viongozi hao kwani wamekuwa wakishuhudia maeneo hayo yakiuzwa
kwa matajiri wenye fedha zao bila wananchi kuhusishwa ikizingatia kuwa maeneo
hayo yalitolewa na wananchi kwa ajili ya huduma za kijamii.
“Haya maeneo tuliyatoa sisi wananchi
kwa ajili ya kujenga shule, zahanati, soko na mambo mengine kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi lakini chakushangaza viongozi hawa wanauza kinyemela tena
kinyume na taratibu, hivyo tunaamua kugawana hapa,” alisema.
Aliongeza kuwa wamefanya jitihada
mbalimbali zikiwa pamoja na kwenda Wilayani kuripoti matukio hayo kwa nyakati
tofauti na wakati mwingine kufikia hata makubaliano yakuendeleza maeneo hayo
lakini kadri siku zinavyokwenda maeneo yanazidi kuuzwa.
Naye Katibu wa Kamati hiyo, Samweli
Kisoma alisema Serikali ya kijiji imeshindwa kuwasikiliza na hata walivyokwenda
wilayani pia wameshindwa kuwajibika hivyo maamuzi yao ni kugawana mashamba hayo
kila mwanakijiji achukuwe kilicho chake.
Akijibu tuhuma hizo za wananchi wake
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ramadhani Mohamed alisema utaratibu wanaoutumia
wananchi hao haukubaliki na wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Alisema mambo wanayoyaleta kijijini
hapo ni ya kisiasa hivyo Serikali ya kijiji itawachukulia hatua wote wanaofanya
vurugu hizo ikiwa pamoja na kushawishi watu wengine kwani wanajulikana.
“Mnajua wanaofanya mambo haya
wanajulikana na mimi kama mwenyekiti sitakubali vurugu hizi na tutahakikisha
tunawachukulia hatua kali wananchi hawa ambao wanahatarisha amani ya kijiji
chetu,” alisema.
Aliongeza kuwa kuna kundi la watu
ambalo linaongozwa na mwenyekiti ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya
kijiji hiki na alitolewa na wananchi hao hao kwa tuhuma mbalimbali na hata
mambo hayo ya kuuzwa kwa ardhi yeye alihusishwa huko nyuma.
“Nadhani anachofanya hapa ni
kuhamasisha wananchi kufanya vurugu hizi, sasa lazima wachukuliwe hatua kali za
kinidhamu ili kukomesha vitendo hivi vya utovu wa nidhamu,” alisema.Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Ahmed Kiponzi aliagiza kukamatwa
kwa wananchi hao nakuongeza wanachokifanya hakikubaliki katika nchi
inayoongozwa kidemokrasia
No comments:
Post a Comment