21 December 2010

Kikwete, Hoseah watajwa WikiLeaks

*Hoseah adaiwa kumchongea Kikwete Marekani
*Ni kuwa anakwepa kushtaki mapapa wa rushwa


Na Mwandishi Wetu

SIRI ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kushindwa kuwaburuza mahakamani mapapa wa
rushwa imefichuka kuwa ni kutokana na Rais Jakaya Kikwete kukosa nia ya dhati ya kuwachukulia hatua kutokana na tabia ya kulindana, mtandao wa WikiLeaks umeeleza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mtandao huo unaovujisha siri za Marekani na kukaririwa na Gazeti la The Guardian la Uingereza jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt. Edward Hoseah alisema hayo alipokutana na Mwanadiplomasia wa Marekani, Purnell Delly Julai, 2007 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa WikiLeaks Dkt. Hoseah aliweka wazi kuwa ili kutekeleza wajibu wake, tuhuma za rushwa zinazomhusu Waziri Mkuu na Rais haziwezi kuwekwa wazi.Anadaiwa kusema pia kuwa viongozi waliopata na watu waliokaribu na kiongozi huyo hawashikiki.

"Rais Kikwete hana nia ya wazi kuacha sheria ifuate mkondo kuendesha kesi za watuhumiwa wa rushwa ambao ni vigogo serikalini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa "Hataki kuonesha mfano mbaya kwa viongozi wastaafu."

Katika mazungumzo hayo, inaelezwa kuwa Dkt. Hoseah alionesha kuhofia maisha yake na kuomba ulinzi wa Marekeni kutokana na ujumbe mfupi wa simu za mkononi na barua alizopokea zikitishia maisha.

"Alisema (Dkt Hoseah) maisha yake yalikuwa hatarini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya mtandao na kuongeza kuwa "vigogo wa kisiasa katika nchi za kiafrika hawaguswi".

Hata hivyo, tayari Dkt. Hoseah amekanusha kutamka maneno hayo, akidai ofisa huyo wa ubalozi alimnukuu vibaya.Kwa mujibu wa mtandao huo, Dkt. Hoseah alizungumza kwa woga kuhusu uwezekano wa yeye kutekeleza nia yake ya kweli dhidi ya vita vya rushwa nchini na kuweka wazi kuwa kuwashughulikia mapapa wa rushwa ni kazi ngumu na kwamba hawatakiwi kuguswa wao na watu walio karibu nao.

Taarifa hiyo ya siri ilisema Dkt. Hoseah aliweka wazi kuwa kulikuwa na kila dalili ya rushwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwamba tatizo hilo ni kubwa pia kwa upande wa Tanzania visiwani.

"Kuna fununu kwamba rushwa iko katika Benki Kuu ya Tanzania na visiwa vya Zanzibar navyo vinanuka rushwa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyonukuu Dkt. Hoseah.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa viongozi wa Zanzibar, ambao baadhi yao walikuwa wakilipwa mishahara na wawekezaji, pia walikuwa wameanza kujiingiza kwenye ufisadi wa kujilimbikizia ardhi.

Taarifa hiyo pia ilizungumzia kesi ya rushwa ya rada ya Tanzania iliyosikilizwa jana katika mahakama moja mjini London nchini Uingereza ikihusisha kampuni ya BAE na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Andrew Chenge.

"Kila aliyehusika na tuhuma hii na BAE nchini Uingereza amewajibika lakini Tanzania wanakwepa kwa sababu kwenye uchunguzi huo halikujitokeza neno rushwa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.Taarifa hiyo ilisema Kampuni ya BAE ilitozwa faini ya dola za Marekani milioni 30 na Taasisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Uingereza (SFO).

"Kuna wakati aliyekuwa Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Afrika, Bi. Clare Short alisema "ni wazi ilikuwa ni mradi wa kipumbavu wa rushwa," ilisema taarifa hiyo.Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa tuhuma za rada zingeweza kushughulikiwa na TAKUKURU pia kwa upande wa Tanzania kwa kuwa Dkt. Hoseah alikaririwa akisema kuwa zilihusisha maofisa kutoka Wizara ya Ulinzi wakiwemo maofisa wa Jeshi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Dkt. Hoseah anapokutana na wafanyakazi wa Taasisi anayoongoza katika vikao vya ndani anakuwa na wakati mgumu kwa kuwa wanamuona kama wamemweka wao.Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Tony Blair, mwaka 2006 aliagiza SFO kufanya uchunguzi kuhusu malipo yaliyofanywa na BAE kwa familia ya Mfalme wa Saudia.Taarifa hiyo ilisema Wizara ta Sheria ilienda mbali zaidi na kuagiza Kampuni ya BAE kulipa faini ya dola milioni 400 sawa na Euro 260 chini ya Sheria ya rushwa ya kimataifa ya US.

Tanzania ilinunua rada ya kijeshi kutoka Kampuni ya BAE kwa garama ya Ero milioni 28 mwaka 2001 kwa ajili ya ulinzi pamoja na kusaidia masuala ya anga.

Baadhi ya washirika wa misaada kama Benki ya Dunia waliweka wazi kuwa gharama za kununua chombo hicho ilikuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotakiwa.Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Dkt. Hoseah jana mchana licha ya kukiri kufanya mazungumzo na ofisa balozi huyo ilipingana na taarifa za Wikileaks na kueleza kuwa Ofisa huyo alimkariri vibaya kwa sababu znazozijua mwenyewe.

"Kwa mfano sikusema kuwa Rais Kikwete ananikwamisha, nilichosema ni kuwa Rais hataki kigogo wa Serikali au mtu yeyote ashtakiwe kwa majungu au bila ushahidi wa kutosha, kwani kwa kufanya hivyo serikali itakuwa hatarini kulipa fidia ya fedha nyingi iwapo mtuhumiwa atashinda kesi mahakamani,” alisema Dkt. Hoseah katika taarifa yake.

Kuhusu kudai maisha yake kuwa hatarini kutokana na mapambano ya rushwa kuhusishwa vigogo na matajiri Mkurugenzi huyo, alikiri hilo na kuongeza kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa kazi yake kama Mkuu wa TAKUKURU anayepambana na vigogo na matajiri.
Nakumbuka ofisa huyo aliniuliza kama ninahofia maisha yangu kama Mkuu wa TAKUKURU au siyo, jibu langu lilikuwa rahisi na wazi kuwa ndiyo. Unapowashughulikia watu maarufu na matajiri ni lazima uwe makini na maisha yako,” alisema Dkt. Hoseah katika taarifa hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo ilikanusha Dkt. Hoseah kutaka kukimbia nchi kwa sababu maisha yake yapo hatarini na kuongeza kuwa anashangaa jinsi alivyonukuliwa vibaya na ofisa huyo wa ubalozi.

Alisema usaliti na kupigwa vita ni sehemu ya maisha yake kwa kuwa anashughulika na watu wenye nguvu na kuongeza kuwa hana wasiwasi kwa kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na bunge na kwamba hakuna aliye juu ya sheria.

26 comments:

  1. Saidmsemakweli......

    Hoseah, hiyo ndiyo faida unayopata kwa kuwabeba mafisadi papa, na nyangumi ambao mtanzania mpigani nchi yake Mhe.Mengi aliipigia kelel mara nyingi lakini kwa sababu ya kubebana imewafikisha hapo!!!!

    ReplyDelete
  2. Hosea wacha majibu ya ujanjaujanja we kubali kubali kuwa ukweli ndo huo kuwa mabosi wako ndo wanakukwamisha...

    ReplyDelete
  3. hii wikileak itatusaidia sana kuwajua hawa jamaa walijivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Kama JK alivyo, akiongea unasema kweli jamaa ana nia ya dhati, but he is the most hypocrite person in TZ. i hate him

    ReplyDelete
  4. Mungu ambariki sana Jullian Assange final tunaanza kuona mkweli nani na mnafiki nani? Ila sioni sababu ya balozi wa marekani kukusingizia uongo maana tumeona jinsi kesi za EPA,Mramba,Yona,Richmond,hata sasa dowans kuwa ni sanaa tupu kama ni ukweli wacha ukweli na dunia nzima ijue nani anatutafuna.Wacha ujanja si unajua wikileaks bado wana release siri utasema nini zikitoka zingine wakati Assange hakujui wala huna alichonacho yeye.

    ReplyDelete
  5. Haya Tumsubiri JK naye atasemaje kuhusu hilo au ndo Hosea naye ataondolewa kama Tido Mhando!! Au atakufa uongo kama yule Gavana. Mmmh kweli Tanzania yetu inaelekea pabaya. Rais mnafiki na viongozi wengi wa serikali ni uozo tu wanalinda maslahi yao binafsi wakati wanainchi tunateseka. Wikileaks imetufungua macho na bado ndo kifo cha mafisadi na aibu zao kimeanza. kaeni chonjo siku za mwisho zimekaribia.

    ReplyDelete
  6. hivi watu kama kina Asange walikuwa wapi siku zote? tunahitaji kina asange kwa maelfu, halafu tuone nani atakana alichosema au fanya! Hongera sana Asange! kila siri iliyovuja inakanwa! ama kweli yote yafanywayo sirini hufichuliwa hadharani!

    ReplyDelete
  7. Tuwaalike WikiLeaks watusaidie kuwabamba hawa mafisadi wa TZ hasa walioko BOT, mabenki, na mashirika ya umma

    ReplyDelete
  8. Utendaji wako Hosea umepitwa na wakati, hakuna siri sasa dunia hii. Kuhusu Kesi BAE inayounguruma sasa hivi london utasema ni uongo. Wakati ulimsafisha Chenge. Mbio za sakafuni daima huishia ukingoni. Heshima yako na Bosi wako imeshuka sana.

    ReplyDelete
  9. Hizi ndio siasa zetu za hakuna kusalitiana na ukitusalitiu tunakuondoa kwenye system, tumeoyaona kwa akina sita na tido mhando. Serikali yetu ipo madarakani kumtumikia nani kama mafisadi wachache ndio wenye thamani zaidi kuliko mamilioni ya watanzania hohehahe?

    ReplyDelete
  10. Huu ndio ujamaa ulio jengwa TZ. AIBU!!!!AIBU!!!!AIBU!!!!. Sasa huyu Rais atazubutu kuongea kitu chochote kuiwakilisha TZ. Wenzake watamsanifu tuu. Unyonyaji unakuvua utu wako. Ufisadi unakuvua utu wako. Rais kilichopo ruhusu mchakato wa katiba ili sheria ichukue mkondo wake.

    Tanzania tuna heshima lakini mafisadi na kulindana inatushushia heshima kiasi ambacho huwezi kutoa ushauri sehemu yeyote. Ni nani atahitaji ushauri wako wakati nyumbani kwako kumeoza.

    Na wewe HOSEAH ni mnafiki, huo mtandao unaujua wa kuzibana mdomo na wewe umo. Na ndio maana unawakumbatia hao mafisadi. Mlimkosa Mh Sitta sasa itakula kwanu.

    ReplyDelete
  11. MSEMAKWELI-NI-MCHA-MUNGUDecember 21, 2010 at 2:11 PM

    Ninawaomba watanzania wenye habari nyeti za serikali kama hizi wapazipeleke Wikileaks. Nadhani hili gazeti lingekuwa la Bongo lingeshafungiwa tayari. Angalia watanzania walivyo wajinga tumewaambia tusichague mafisadi lakini kutokana na uelewa wao mdogo na nguvu za mafisadi wamewasharudisha madarakani na wanaanza kupandisha bei ya umeme na mafuta yatafuata. ACHA WATANAZNAIA WA KI KIZAZI HIKI WAFE WOTE NDIO WATAJUTA KUWACHAGUA MAFISADI, LABDA KIZAZI KIJACHO KINAWEZA KUNG'AMUA.

    ReplyDelete
  12. Mheshimiwa achana uzinduzi wa Mahoteli ya kifahari kemea hayo mafisadi wanakuabisha. Kama kweli msafi na wanyooshee kidole lakini kama si msafi endelea kunyamaza tu. Au kwa kuwa ndo ngwe yako ya mwisho. kumbuka unawekea wakati mgumu mgombea anayekuja wa ccm, labda achakachue kama mlivyozoea ndo apite. hampiti tunawahikishieni 2015, mfanya maisha yamekuwa balaa. Muondoeni na huyo kama tido mhando, sita na mbunda kwa ufisadi wenu.

    ReplyDelete
  13. Judge questions BAE deal over payments for Tanzania contract
    Mr Justice Bean tells Southwark Crown court it appeared that BAE had paid 'whatever was necessary' to get contract BAE has steadfastly argued that it did not make corrupt payments to secure a contract from the Tanzanian government. Photograph: Murdo MacLeod for the Guardian. A controversial deal between prosecutors and Britain's biggest arms firm, BAE, was today challenged by a judge who said the company appeared to have been engaged in bribery. BAE had reached a deal with the Serious Fraud Office earlier this year in which it agreed to plead guilty to a relatively minor accounting offence. BAE steadfastly argued that it did not make corrupt payments to secure a £28m contract from the Tanzanian government. But today, Mr Justice Bean questioned the heart of the agreement, repeatedly saying that payments originating from the company appeared to be "corrupt" and for "bribing decision-makers in Tanzania". He told Southwark crown court that it appeared that BAE had paid "whatever was necessary to whomever it was necessary" to get the Tanzanian contract. He added that it appeared that the payments were disguised so that BAE "would have no fingerprints on the money". "They just wanted the job done – hear no evil, see no evil," he said. The judge is due to sentence BAE tomorrow. In February, BAE struck the plea deal with the SFO and American prosecutors to end years of corruption investigations into its business methods. The arms giant agreed to pay £30m in corporate penalties in return for admitting accounting irregularities over a radar contract with Tanzania. Anti-corruption campaigners have argued that the deal is too lenient and cosy. Today, Victor Temple, the QC for the SFO, told the court that BAE had set up a system of "covert" and "overt" agents to sell their arms around the world. The "overt" advisers "conducted their work openly as BAE's in-house representatives", he said, while the "covert" agents' work was "highly confidential". He said Sir Richard Evans, BAE's chairman, had "personally approved" the use of a businessman, Sailesh Vithlani, as its "covert" agent to secure the Tanzanian radar contract.He said: "I have to establish what has happened. If there is no money to be used for corrupt practices, why is 97% of it paid through a BVI company controlled by BAE to another [offshore] company controlled by Vithlani?" When Temple said Vithlani had been hired to lobby for BAE, the judge questioned why the businessman was paid so much for his work. Temple said that lobbying was legitimate work. "To lobby is one thing, to corrupt another". Temple added that BAE had committed the accounting offence as Vithlani had been recorded in its books as performing "technical services", but he had no knowledge of any technical matters. David Perry, QC for BAE, argued that the firm had not admitted any corruption and should only be sentenced for the one offence they had confessed to in the plea bargain. The judge had threatened to call witnesses to testify as he wanted to established the purpose of the payments, but later decided to go ahead with passing sentence tomorrow.

    ReplyDelete
  14. Fundi mitambo wa Majira

    Hebu boresha mtandao wako kwa kuweka self generating Anonymous 'numbering' ili afahamike kwa ufasaha Anonymous aliechangia.

    Wakati mwengine tunataka kumsapoti au kumpinga Anonymous aliechangia lakini inakuwa tabu kumu-identify

    ReplyDelete
  15. kwa kifupi kashfa hii inaonyesha kwamba watanzania hawana kiongozi na kwa watanzania wanayo bado ufahamu yaani wana akili timamu ni wakati wa kuwalazimisha wajiuzulu hamna haja ya katiba kwani wakiweko bado wataivuruga. Enyi watanzania mnaelewa au nirudie tena? wabunge wenu wanatakiwa leo hii wapige kura ya kutokuwa na imani na raisi na jopo lake la sivyo hao wabunge waelewe wazi kuwa hawakujiweka wao kwenye ubunge.

    ReplyDelete
  16. Tiba ya haya yote ni kuwa na katiba itakayoweka maslahi ya nchi yetu mbele badala ya masilahi ya kikundi kidogo yaani rais na wateule wake. Fikiria hata kama upo ushahidi kwamba Mkapa alijilimbikizia mali kinyume na sheria eti hawezi kushitakiwa kwa kuwa aliwahi kuwa raisi ya nchi. Hata kama upo ushahidi kwamba alituibia sana kwa kutumia wadhifa wake hawezi kushitakiwa! Du kweli Tanzania ni nchi ya ajabu sana ambayo sijapata kuona sehemu yeyote ya dunia. Nijuavyo raisi kweli asishitakiwe kwa makosa aliyoyafanya kwenye maamuzi yake kama rais, endapo kwa bahati mbaya alifanya uamuzi usio na manufaa juu ya swala lolote hiyo sawa. Lakini si uamuzi wenye maslahi yake binafsi. Kama kuuziwa nyumba kwa kigezo cha utumishi wa serikali, au mashamba ya miwa kule Mtibwa, Kilombelo na maeneo mbalimbali ya Tanzania aliweza kujichukulia na kuwaacha wananchi maskini kwenye lindi la umaskini. Na wakati huo huo kodi zetu zinamtunza mpaka kufa kwake! Hivi kweli hiyo ni haki jamani. Tumewapa marais wetu bonasi kubwa ili wasiingie kwenye majalibu ya kutuibia lakini bado kwa mtu kama Mkapa imekuwa bure kabisa. Ndo anajilimbikizia mali kwa ajili ya watoto wake ili waishi peponi. Chonde chonde Kikwete ruhusu mchakato wa katiba ili tuondoe uozo huu. La sivyo tutakuwa na mashaka na wewe kwamba unania ya kutumia kipindi chako cha mwisho kujitajirisha wewe na mwanao Riwadh. Usiporuhusu nguvu ya umma itakuja kuwawajibisha wote mlituibia utajiri wa nchi yetu kwa faida yenu pekee yenu eti kwa kuwa tuliwapa dhamana ya kutuongoza tena kwa kuchakatua matokeo. Wezi hawawezi kudumu hata siku moja.

    ReplyDelete
  17. Tanzanian need to wake up,your Leaders in the Goverment been treatening us like a piece of SHIT,
    Today Tanzanian whatever your got no fucking value,respect even our deginity has gone because of this Fucking Corrupt President with his fucking corrupt ministers.we must train and go dump that goverment rotten in jail.god bless Tanzanian .AMEEN

    ReplyDelete
  18. YOU PRESIDENT Kikwete your responsibility with our life,and even a blind person can see what type of your gorvement is,carry on like that cause is the way you planned to run this beautful country in CORRUPTION AND VANDALISING,
    But you must nt forget that there is ONE DAY,
    YOU AND YOUR MINISTER ARE GOING TO PAY WITH HIGH PRICE.NOT IN HEAVEN HERE IN TANZANIA

    ReplyDelete
  19. Majira mnaanza kuchakachua maoni hamna sababu ya kuondoa maoni ya mtu. Mwenye ushahidi wa ufisadi akafungue kesi yeye. Kikwete hakukosea kumwambia Hosea asifungue kesi kwa kusikiliza anayosema mtu,hapa pana kosa gani? huko mahakamani panatakiwa ushahidi usio shaka na hao wazungu siku zote wanataka sheria ifatwe,sasa huyu Hosea kama naye kalishwa na mafisadi asimsukumie boss wake,kwani inashangaza kesi ya kina Mramba hadi sasa hakieleweki kinachoendelea zaidi ya kesi kuahirishwa.

    ReplyDelete
  20. Who is a fucking corrupt president? Kikwete or Mkapa. Who destroy our country economy? Did Kikwete sell any gold,tanzanite mines since he became a president.RADAR, TRC,HABOUR,GOLD MINES,TANZANITE,GOLD MINES,TANESCO,BOT SCANDALS,ATC and many others scandles are they product of Kikwete? dont be selfish. (kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe)

    ReplyDelete
  21. Nyie MAJIRA kweli mnachekesha, maoni yetu mnayaondoa kwa sababu tuasema ukweli, wala hatuwashangai, ondoeni lakini ujumbe tumeufikisha. Tunajua hili ni gazeti la rightwings ndio mrengo wenu na eti mwalilia haki na demokrasia wakati nyie vimewashinda. Hivi kweli mtu mzima unakaa unachambua kuwa haya maoni hayajanipendeza au hayajaelekea kule ninakotaka mimi kisha unayatoa, kweli bado safari ndefu mnayo, jifunzeni kutoka kwa magazeti ya nje yaliyo kwenye mtandao maoni yanafika mpaka 300 tena yenye different views. Mtu mwenye uelewa na upeo atashangaa nchi nzima kuwa na maoni ya kufanana unless mnakaa wenyewe chini na kuyaandika, hamna kazi ati!

    ReplyDelete
  22. Inasikitisha kuona baadhi ya ndugu zetu wanatoa matusi na lugha za kihuni hapa mtandaoni. isitoshe kama wale wachangiaji ambao ni mabingwa wa kimombo hapa sio pahala pake maana sisi ni waTz na tunajivunia lugha yetu ya kiswahili.

    Pia Kumtukana Kikwete au viongozi walochaguliwa kitaifa ni kukosa heshima, ustaarabu na upevu wa kiakili. Hujalazimishwa kuchangia. na iwapo umezoea uhuni hapa sio pahala pake. Jibu au toa mawazo yahusuyo mada zitolewazo na uwache tabia au kuleta matusi hapa. Tz, watu wake inaheshimiwa sana wakiwemo viongozi wake pia. Jiheshimu na watu ulimwengu ukuheshimu.

    ReplyDelete
  23. Ndugu Mhariri wa Majira,mimi ninachoona katika utoaji wa maoni haya ni kwamba kuna watu wanajifanya kuwa ni wakereketwa wakuchangia hoja lakini kumbe wao ni mafisadi walewale.NASEMA KUWA SERIKALI ILIYO MADAKANI IJIPIME YENYEWE.

    Kimali, BJ

    ReplyDelete
  24. Kilimali, tupo pamoja kaka. hata hivo uzuri wa mtandao huu ni kutoa fursa kwa kila mmoja atoe joto lake. mafisadi wametuzunguka katika jamii yetu kila upande.

    mpaka tutapoweka masilahi ya wananchi mbele na kuheshimu sheria tulizojiwekea, mafisadi wataendelea kuzaliwa tu.

    ReplyDelete
  25. Bwana hosea kwa hali halisi ya jinsi rushwa inavyojengeka tanzania ni aibu kwa sisi tunaoishi hapa USA.Alichosema bwana kutoka marekani sio uzushi wara majungu wewe na rais kikwete ni lenu moja kuwakumbatia mafisadi na inawezekana nyie ndio mnaomiliki DOWAN.Mnaogopa nini ulinzi na vitu vyote mnavyo uganga wa kienjeji mnao watoeni hawa watu hadhalani jamii ijue.

    ReplyDelete
  26. Inashangaza majira mnachakachua maoni lakini yale yanayomtukana Rais wa jamhuri ya Tanzania mnaayaacha kama vile huyo aliyeandika fucking president Kikwete, tunapowasema wachaga na tabia zao unachakachua sijui uliop hapo ni mchaga?

    ReplyDelete