19 September 2013

WABUNGE NIGERIA WATWANGANA MAKONDE ABUJA, Nigeria
WABUNGE nchini Nigeria wamerushiana makonde baada ya kundi lililojitenga kutoka chama tawala cha PDP kujaribu kuhutubia Bunge.Bunge hilo la chini lilifanya vikao baada ya mapumziko ya wiki saba - ambapo kundi jipya la PDP liliundwa.

Kwa mujibu wa BBC, Wabunge ambao ni watiifu kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria walianza kupiga kelele na kuzomea, ambapo kitendo hicho kiliwaudhi wapinzani wao na ndipo mtafaruku ulipoanza.
Kundi hilo lililojitenga linapinga Rais Jonathan kuwania kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa 2015.
Bw. Jonathan bado hajasema kama atagombea, lakini baadhi ya washirika wake, akiwemo mkewe, wameanza kumfanyia kampeni.Kulingana na BBC, Mbunge mmoja alionekana akimchania shati mwenzake katika hali ya vurugu ndani ya Bunge la Wawakilishi la Nigeria mjini Abuja.
Ugomvi huo ulidumu kwa dakika 10 huku Wabunge wakitwangana makonde.Picha za televisheni z i l i o n e s h a Mb u n g e mwanamke akimtia kidole mwenzake usoni. Mbunge mwingine alionekana akichukua kiti katika kujaribu kumpiga mtungasheria mwenzake, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.
C h a m a c h a P D P kimekuwa kikishinda chaguzi tangu kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, kwa maana hiyo mgombea urais wa chama hicho atakuwa katika nafasi nzuri kuwa kiongozi atakayefuata wa Nigeria.Bw. Jonathan amekuwa rais tangu 2010, wakati mtangulizi wake alipokufa na akapandishwa kutoka makamu wa rais hadi kuwa rais.

1 comment:

  1. Watanzania wanavyopenda kuiga wakisoma hili wataongeza kasi ya kutukana na kuchapana makonde bungeni. Sugu soma hapa papa ukatunishe msuli vizuri

    ReplyDelete