Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete,
ameshangazwa na kiwango cha uongo wa baadhi ya wanasiasa na hasa madai kwamba
aliteua wajumbe wa Tume ya Katiba bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau
mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa bado anaendelea kuamini kuwa
mchakato wa Katiba Mpya utafikia mwisho wake mwakani, 2014, na hivyo kuiwezesha
Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 chini ya Katiba Mpya.
Rais Kikwete aliyasema hayo Jumatatu, wiki hii, mjini San Rafael,
California wakati alipokutana na kuzungumza na Jumuiya ya Watanzania waishio
Jimbo la California, nchini Marekani, wakati alipoanza ziara yake ya siku mbili
katika Jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Marekani.
Vilevile, Rais Kikwete alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera
za Serikali au hata kumpinga yeye binafsi bali tatizo lake ni wanasiasa na
wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.
"Watu wote niliowateua walipendekezwa na wadau mbali mbali
zikiwamo taasisi za dini. Yule Mama Maria Kashonda alipendekezwa na Baraza la
Maaskofu Tanzania (TEC), Mama Mwantumu Malale alipendekezwa na Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (BAKWATA). Kila kundi ambalo lilipendekeza watu limepata mjumbe katika Tume
hiyo wakiwemo walemavu ambao naambiwa nimewasahau," alisema Rais Kikwete
na kuongeza:
"Hivi nyinyi wanasiasa wenzangu mkikosa hoja mnaongopa hata
kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa. Tulikubaliana kuwa Rais angefanya uteuzi wa
wajumbe wa Tume baada ya kupokea mapendekezo ya wadau mbali mbali na katika
mchakato ulioendeshwa kwa uwazi kabisa. "Hivyo, ndiyo ilivyofanyika. Sasa uongo wa nini? Kama hakuna
hoja ni kwamba hakuna tu na wala uongo hautasaidia."
Kuhusu mjadala wa karibuni kuhusu kama Rais awe na madaraka ya
kuteua wajumbe 166 wa nyongeza ili kuingia katika Bunge la Katiba kujadili
Rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete amesema kuwa yeye hana tabu kama itabidi
ateue basi atateua, lakini kama si lazima yeye hatafanya hivyo.
"Mimi sina taabu, wakisema niteue basi nitateua. Wakisema
nisiteue vilevile sina taabu, isitoshe hiyo itakuwa inanipunguzia mzigo na
kazi. Ile
kazi yenyewe ya kuteua Wajumbe wa Tume ya Katiba ilikuwa siyo rahisi
No comments:
Post a Comment