LIVERPOOL, Uingereza
MANCHESTER United jana ilichezea kichapo
cha bao 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool.Mechi ilianza
kwa Man United kulifikia lango la Liverpool lakini mabeki wa Liverpool
walisimama imara kuondoa mashambulizi hayo.
Liverpool
ilipata bao lake dakika ya nne kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani kwa
kichwa na Daniel Sturridge akimalizia mpira wa krosi kutoka winga wa kulia.Dakika ya sita
nusura Robin Van Persie aipatie Man United bao kwa tiktak, lakini shuti lake
lilipaa juu ya goli.
Dakika ya tisa Man United waligongeana
pasi vizuri lakini shuti la Danny Wellbeck lilidakwa kiustadi na kipa wa
Liverpool.Kipindi cha pili Man United waliingiwa
na uchu wa kupata mabao, ambapo dakika ya 46, 49 na 53 ilipata kona tatu
mfululizo ambazo, hata hivyo, hazikuzaa matunda.
Dakika ya 71 Nemenja Vidic nusura
angeizawadia bao Liverpool baada ya kurudisha mpira fyongo kwa kipa wake David
Degea ambao uliwahiwa na mshambuliaji Coutinho ambaye hata hivyo alishindwa
kufunga.Licha ya washambuliaji wa Man United Luis Nani,
Wellbeck, Chicharito, Ashley Young na Valencia kuwa na uchu wa mabao lakini
kikwazo kikubwa kilikuwa kwa kipa wa Liverpo
No comments:
Post a Comment