- JESHI LASISITIZA HAKUNA KURUDI NYUMA HADI MWISHO
- MAGAIDI SITA WAUAWA,10 WAKAMATWA AIRPORT
NAIROBI, Kenya
Hali si shwari, unaweza kusema hivyo
kutokana na mapambano yanayoendelea ndani ya Jengo la Westgate, nchini Kenya, kati ya
majeshi ya Serikali nchini humo na magaidi wenye silaha tangu Septemba 21 mwaka
huu
. Jengo
hilo lilivamiwa na wapiganaji wa Al Shabaab
ambao wanadaiwa kufikia 10 hadi 15, kusababisha mauaji ya watu 62, wengine 175
kujeruhiwa na kuwateka baadhi ya watu ambao hadi sasa wanawashikilia ndani ya
jengo hilo.
Jeshi
la Polisi nchini, limesema watu 10 wanashikiliwa na walikamatwa wakati
wakipanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).Pia
jeshi hilo limewaonya Wakenya dhidi ya utapeli
unaofanywa na baadhi ya watu wanaochangisha fedha ili kusaidia waathirika
ambapo utoaji damu bado unaendelea Uhuru
Park, jijini Nairobi.
Taarifa
iliyotolewa na Kituo cha Televisheni cha Citizen nchini humo, kilisema magaidi
sita wameuawa katika mapambano hayo na wengine waliobaki ndani ya jengo hilo, wanaweza
kujisalimisha baada ya kuwazidi nguvu.
Kituo
hicho kimeongeza kuwa, wanajeshi watatu wa Kenya
kati ya 11 waliojeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea ndani ya jengo hilo, wamefariki dunia na
kubaki wanane.Mkuu
wa Majeshi nchini humo, Jenerali Julius Karangi, alisema katika mapambano hayo
hakuna kurudi nyuma hadi magaidi hao wajisalimishe wenyewe.
Raia
wa nchi nyingine wahusishwa
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje nchini Kenya,
Bi. Amina Mohamed, amesema mwanamke mmoja raia wa Uingereza anadhaniwa kuhusika
na tulio hilo.Bi.
Mohamed alisema, mbali ya mwanamke huyo pia kuna raia wawili au watatu
Wamarekani ambao inasemekana ni miongoni mwa magaidi hao wa mtandao wa Al
Shabaab.
Kwa mujibu wa Shirika
la Utangazaji la Uingereza (BBC), lilisema raia sita wa Uingereza
wamethibitishwa kufa katika shambulio hilo.Ofisi inayohusika na
Mambo ya Nje nchini Uingereza, ilisema ndugu wa karibu wa raia hao ambao
wamepoteza maisha katika shambulio hilo,
tayari wamepewa taarifa.
Pia ofisi hiyo
ilifafanua kuwa, haina taarifa zozote juu ya raia wao kuhusika na shambulio hilo, lakini bado wanaendelea kushirikiana na mamlaka za Kenya ili kuwasaidia katika uchunguzi kutokana
na shambulio hilo
la kinyama.
Akizungumza na
waandishi wa habari nchini Pakistan,
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Theresa May, alisema "Nimepata
taarifa kuwa mwanamke raia wa Uingereza amehusishwa na tukio hili."Tutathibitisha
taarifa hizi kama uchunguzi utakamilika, si
rahisi kukubali au kukanusha kwa sasa," alisema May.
Jeshi
la Kenya
Hadi jana mchana,
Jeshi la Kenya lilikuwa
katika hatua za mwisho kukamilisha msako wa kulikomboa jengo hilo mikononi mwa magaidi.Shirika la Habari
nchini Ufaransa (AFP), lilisema majeshi ya Kenya
yalikuwa yakikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa magaidi wawili walioosalia
ndani ya jengo hilo
kila mmoja akiwa amejificha eneo lake.
Milio ya risasi na
milipuko ilisikika jana asubuhi katika jengo hilo,
lakini Serikali ya Kenya,
haijatoa idadi kamili ya mateka waliookolewa katika shambulio hilo.Kwa mujibu wa Kituo
cha Televisheni cha K24 nchini Kenya,
jana kilitangaza majina sita ambayo ni miongoni mwa magaidi wanaodaiwa kuhusika
na shambulizi hilo.
Washukiwa hao ni Sayd
Nuh (25), anayetoka Kismayu, Isamil Galed (23), Finland, Mustafa Noordiin (24)
na Abdifatah Osman (24) wote raia wa Marekani, Kassim Musa (22), Garissa na
Mohammed Badr (24), ambaye ni raia wa Syria.
Al
Shabaab ni nani?
Jina Al-Shabab
linamaanisha kijana kwa lugha ya Kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama
za Kiislamu ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006 baada ya kupigana na wanajeshi
wa Ethiopia waliokuwa
wameingia nchini Somalia
kuyaunga mkono majeshi ya Serikali.
Kundi hilo limeweka sheria kali
za Kiislamu katika maeneo wanayoyadhibiti ikiwemo ya kupigwa mawe hadi kufa
wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati na kuwakata wezi mikono.Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti katika baadhi ya miji mikubwa
nchini Somalia,
liliondoka Mji Mkuu Mogadishu Agosti 2011 na Mji wa Kismayo Septemba mwaka
2012.
Kismayo ulikuwa mji
muhimu wa kundi hilo
na uliwawezesha kufikiwa na bidhaa pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli
zao.Kundi hilo lilianza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya
kushindwa na Majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao ambapo Kenya
ilianza harakati za kulimaliza kundi hilo
mwaaka 2011 Kenya
iliwatuhumu wapiganaji wa Al Shabaab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja
na watalii.
Nani
kiongozi wa Al-Shabaab?
Ahmed Abdi Godane
ndiye kiongozi wa kundi hilo ambaye anajulikana
kama Mukhtar Abu Zubair, akitokea katika Jimbo la Somaliland.
Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo, zinapingwa vikali na
kundi lenyewe.
Kiongozi wa kundi hilo Godane huwa
haonekani hadharani, ambapo mtangulizi wake, Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa
katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.Al Shabaab walijiunga
na al Qaeda, Februari mwaka 2012, ambapo kiongozi wa Al Shabaab (Godane),
aliahidi kumuunga mkono kingozi wa al Qaeda, Ayman al-Zawahiri. Makundi hayo mawili
yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja na baadhi ya raia wa kigeni wamekuwa
wakiweaunga mkono na kuwasaidia katika harakati zao za mapigano
amani ni kitu cha msingi ktk maisha selikari ya kenya ijiratibu juu ya chanzo cha kuvamiwa na magaidi hao, jeshi la kenya hatuna budi kulipongezz mpaka hatua lilipofikia malambi mayenga wa tanzania kahama
ReplyDelete