- YAKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA PIPI 33
Na Frank
Monyo
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewashikilia watu wawili wakazi wa
Tabata, kwa tuhuma za kukutwa na maiti ambayo tumboni ilikuwa na dawa za
kulevya aina ya heroine.Kamanda wa
Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliyasema hayo Dar es Salaam jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema maiti
hiyo ilikuwa na dawa hizo pipi 33 na kuwataja watuhumiwa kuwa ni Nasri Omari
'Roboti' (36) na Mwanaisha Salim (36), wote wakazi wa Kigogo Luhanga, wakiwa na
mwili wa marehemu Rajabu Kadunda.
"Tulipata
taarifa kuwa kuna mtu amefariki ghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni
kuoga... tulikwenda eneo la tukio nyumbani kwa Omari na kuhoji hatimaye
tuligundua uwepo wa maiti sebuleni ikiwa imelazwa chali katika godoro sakafuni.
"Omari
ambaye ndiye mmiliki wa chumba kilichokutwa maiti, alisema marehemu ambaye kwa
jina lingine anafahamika kama Mashaka Mabruki (43) ni mfanyabiashara,"
alisema.
Aliongeza kuwa, uchunguzi unaonesha
kuwa marehemu alifika Dar es Salaam akitokea mkoani Mtwara Septemba 21 mwaka
huu, kwa maelezo kuwa ni mgonjwa na alikwenda kuchukuliwa na watuhumiwa hao
ambapo muda mfupi kabla ya kifo chake, alikwenda bafuni kuoga na hatimaye
kufariki dunia.
Kamishna Kova aliongeza kuwa, mazingira
ya kifo hicho yalisababisha polisi kufika eneo la tukio, kuchukua maiti na
kuipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi. "Uchunguzi uliofanywa na jopo la
madaktari wawili pamoja na Maofisa wa Juu wa Polisi na ndugu wa karibu wa
marehemu, zilikutwa pipi 33 za dawa za kulevya tumboni kwake.
"Pia marehemu alikutwa na hati ya
dharura ya kusafiria nchi za nje ambazo hazikuonesha anasafiri kwenda nchi gani
hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini mtandao mzima wa
usafirishaji dawa hizi uliomhusisha marehemu," alisema.
Alisema zipo taarifa zinazoonesha
marehemu alikuwa mhalifu mzoefu wa kusafirisha dawa hizo kwani kabla ya kurudi
Tanzania alikuwa akitumikia kifungo nje ya nchi Barani Asia.Wakati huo huo,
jeshi hilo l ime f a n i k iwa k umk ama t a Dismas Chacha (33), ambaye ni
mfanyabiashara mkazi wa Tabata kwa kujifanya mtumishi wa umma (daktari).
Kamishna Kova alisema, polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema
kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kuchukua fedha zao akiwa na kawaida
ya kuvaa mavazi ya kidaktari ambapo baada ya kupekuliwa, alikutwa na nyaraka
mbalimbali zenye nembo ya Hospitali ya Muhimbili
No comments:
Post a Comment