06 September 2013

TPB YATANGAZA WASHINDI WA WESTERN UNION



Na Goodluck Hongo

BENKI ya Posta nchini (TPB) imetangaza w a s h i n d i s a b a wa promosheni ya shinda na western union ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia sh.500,000.Akitangaza washindi wa shindano hilo Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa masoko wa TPB Deo Kwiyukwa alisema washindi waliopatikana ni wale waliotuma ama kupokea pesa kupitia huduma ya western union ambapo wamepatikana kutoka ndani ya mikoa mbalimbali
.Alisema jumla ya sh.milioni 1.5 zitatolewa kwa washindi hao ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Sh.500,000, pili atapata sh.300.000,mshindi wa tatu atapata sh.200,000 na katika mshindi wa nne kutakuwepo na washindi watano ambao kila mmja atapata sh.100,000.Bw.Kwiyukwa aliwataja washindi hao kuwa ni Bi. Dora Chopa ambaye ni mshindi wa kwanza,Mwanaisha Shabani ambaye ni mshindi wa pili,mshindi wa tatu ni Sanki Edward ambapo katika kundi la washindi wa nne liliongozwa na Otilia Mchuchula.

“Tunawaomba wananchi washiriki shindano hili kwa kutuma pesa na kupokea kupitia western union kwani hii ni droo ya kwanza, lakini bado kuna nyingine ambayo itachezeshwa mwishoni mwa mwezi wa tisa," alisema Kwiyukwa.Hiyo ni droo ya kwanza t a n g u s h i n d a n o h i l o litangazwe ambapo wananchi wote wanaweza kutuma maombi yao ikiwa watatuma ama kupokea fedha kupitia huduma hiyo ya western union kwa benki nyingi ambazo wanaubia na TPB.Droo hiyo ilihudhuriwa pia na ofisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ambayo inasimamia

No comments:

Post a Comment