Na
Frank Monyo
KAMPUNI ya
simu za mkononi ya Airtel imemtangaza ofisa wa Benki Kuu, Bi. Anna Lyimo (29),
mkazi wa Dar es Salaam
kuwa mshindi wa pili wa nyumba aliyepatikana kupitia promosheni maalumu
inayofahamika kwa jina la Airtel Yatosha shinda nyumba
.Akizungumza baada ya
kuchezeshwa kwa droo hiyo jana Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa
Airtel,Bw.Jackson Mmbando alisema Airtel inayo furaha kuchezesha droo ya pili
ya nyumba ambapo mshindi atapata nyumba ya kisasa ya vyumba vitatu, iliyojengwa
na Shirika la National Housing iliyoko Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Bi.Lyimo
amejishindia nyumba yenye thamani ya sh. milioni 65 na kuwa mshindi wa pili
kushinda nyumba baada ya Bw. Silvanus Juma kuibuka mshindi wa kwanza mwezi
uliopita.Alisema kuwa mpaka sasa
Airtel imetoa nyumba 2 kwa Watanzania huku washindi wengine 56 wakiondoka na
sh. milioni moja kila mmoja.Aliendelea kwa kusema bado
wateja wa Airtel w a n a w e z a k u e n d e l e a kushindania nyumba moja
iliyobaki kwa kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel na mwisho wa siku mtu
anaweza kuibuka mshindi wa nyumba au kushinda milioni moja kila siku.
Ili kushinda mteja
anahitaji kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi cha siku, wiki au mwezi baada
ya hapo mteja atakuwa ameingia moja kwa moja katika promosheni ya Airtel
yatosha shinda nyumba 3, itakayomwezesha kujishindia milioni moja kwa kila siku
au nyumba kwa kila mwisho wa mwezi.Akielezea furaha yake
mshindi huyo wa nyumba B i . L y i m o a l i s e m a : "Ninamshukuru Mungu
kwa bahati hii na noamba Airtel waendelee kuleta mabadiliko kwa wateja wengine
kama walivyofanya kwangu... nimekuwa nikijiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha
k a m a h u d u m a l a k i n i sikuwahi kudhani kama nitaweza kushinda, leo
nimeamini kuwa promosheni hizi zinamlenga mtu yeyote na unaweza kuabahatika
kushinda zawadi kubwa kama hiiĆ®
Airtel yatosha promotion bado inaendelea, nyumba
mbili zenye thamani ya sh. milioni 65 kila moja zimeshazawadiwa kwa wateja na
bado nyumba moja ambayo itatolewa mwezi wa kumi na zawadi ya pesa taslimu kiasi
cha sh. milioni 34 ambazo bado hazijakabidhiwa.Airtel jana imezindua ofa mpya ya kifurushi cha siku
cha Airtel Yatosha BABA LAO kinachomwezesha mteja kuwasiliana na mtandao wowote
nchini kwa sh.499 mteja anapata dakika 20 za muda wa maongezi,sms 300 na
internet MB 125, hii ni ya kwanza na pekee sokoni kutoka Airtel.
No comments:
Post a Comment