06 September 2013

TFF YABURUTWA MAHAKAMANI



 Na Rehema Mohamed
KAMPUNI ya Punchlines Tanzania Limited, imeliburuta katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kudai fidia ya sh. 141,090,464 kwa kukiuka mkataba wa kusambaza tiketi.Kesi hiyo ya madai namba 106 ya mwaka 2013, imefunguliwa mahakamani hapo Agosti 21 mwaka huu, ipo mbele ya Jaji Robart Makaramba na inatarajiwa kutajwa Septemba 12, mwaka huu.

Kampuni hiyo inayowakilishwa na Kampuni ya Uwakili ya BM Attorneys, katika hati yake ya kesi hiyo, kampuni hiyo inadai kiasi hicho cha fedha ikiwa ni pamoja na hasara mbalimbali ilizozipata katika maktaba huo, ikiwa ni pamoja na usumbufu mkubwa kwa wateja wao, kupunguza uaminifu katika benki.
Inadai kuwa TFF na kampuni hiyo, iliingia mkataba huo katika tarehe tofauti kuanzia mwaka 2008 hadi 2011 kwa kufanya kazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusambaza tiketi kwenye mechi mbalimbali kulingana na makubaliano waliyoingia.
Ilibainisha kuwa kati ya mwaka 2008 hadi 2009, kwa mechi za Taifa Stars za Tusker na Vodacom iligharimu sh. 58,092,556, sh. 34,945,110 tiketi za mechi ya Kombe la CECAFA mwaka 2010, Ligi ya Vodacom ya mwaka 2011 sh. 37,467,560 na kwa mechi ya Taifa Stars dhidi ya CAR ya Machi 2011 ni sh. milioni 10,585,238.Iliongeza kuwa TFF imekataa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu zake binafsi.

No comments:

Post a Comment