05 September 2013

NI KIAMA: ATAFUNWA USO NA MWAJIRI WAKE NYUMBANI

 • KABLA ALIANZA KUNG'ATA ULIMI WA MBWA
 Na Waandishi Wetu
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani ukurasa wa mbele.

Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Aliliambia Majira kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma.
“Mshtakiwa huyo alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC Mwamotto wakati wa mahojiano na Majira.
Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza na vipande.
Alisema kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka kwa wingi,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Majira iliendelea na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa mwenzake,” alisema.
Alisema kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,” alisema.
Alisema kuwa pia amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa kujeruhiwa vibaya usoni hali ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba Watanzania kumsaidia kijana huyo ili aweze kwenda kutibiwa haraka nje pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa kuwasiliana na mganga mkuu wa hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri mtendaji wa gazeti hili la Majira

12 comments:

 1. Tanzania imekuwa nchi ya majanga sana, toka kwenye tindikali, mabomu nasasa kutafuna watu. kwa kweli ndugu rais inambidi awe makini katika kutoa elimu juu ya athari za mambo haya kwa jamii. la sivyo tanzania tunaenda pabaya.ni mtazamo tu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Inatisha ulimu wa mbwa unaunyofoa mpaka mbwa kafa anakuja kwa kijana nyofoa macho nyofoa mdomo eh maajabu gani au mwanga?

   Delete
 2. Mh hii hali inatisha mtu anakuwa kama mnyama ,hii siyo kawaida inabidi achunguzwe sana .

  ReplyDelete
 3. Jaribuni kumpima Kichaa cha mbwa huyo mtuhumiwa

  ReplyDelete
 4. Huyo hana kichaa hana chochote ni unyama tu na dawa yake sio kuwekwa Gerezani akiendelea kutafuna sembe akitowelea wenzake.Auliwe huyo asiendelee kujeruhi wenzake.

  ReplyDelete
 5. Kiama hicho. Kwanza ilikuwa vichwa vyenye vipara vikaingia kuchuna ngozi vikaendelea nyeti za watu, vikahamia kwenye kipiga nondo,vikaudi kwa maalbino,vkageukia kwenye tindikali,vikakimbilia kupiga risasi na kufyeka wachungaji mapanga,ikaonekana haitoshi yakaanza mabomu ya hapa na pale,suluhu haikupatikana wakaingilia vikongwe,sasa wameamua kujaribu kula watu huku wakijiona kimacho macho!? Eti jamaani niambieni mnafiri ni nini kinachoendelea nchini? Hivi ni kweli Tanzania ni kisiwa cha amani au cha damu?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Imefikia wakati sasa kila mmoja wetu kumrudia Mungu. Hii ni dalili mbaya, inaonyesha dhahili kuwa baadhi ya binadamu kukosa utu na wamegeuka na kuwa wanyama. Ni wajibu wa kila mmoja wetu sasa kushukuwa nafasi ya kumwomba Mungu ili atuepusha na roho chafu kama hizi. Tumsihi sana Mungu atujaze roho ya upendo na kuishi kama alivyotuagiza, tupendane kama Mungu alivyotupenda sisi. Lakini kwa haya ambayo tunayashuhudia ni dalili ya kutoweka kwa upendo miongoni mwetu.

   Delete
 6. @M.Kimambo;Hilo nalo suala la kusema Rais aanngalie jamani hivikweli hiyo inawezekana!Naona siyo kulaumu uchawi au Ushirikina kuna mengine ni magonjwa ya akili. Hivyo tuchukue tahadhari unapoona jambo siyo la kawaida badala ya kusubiri kuona mwisho wake.

  ReplyDelete
 7. Ingekuwa kiongozi wa serkali au mtu maarufu angeshapelekwa India lakini mtu wa kawaida tena wa kibondo hana hata heshima ya mmbwa wa Ulinzi ambaye akikohoa anapelekwa Nairobi kutibiwa.
  Serkali haswa mkuu wa wilaya alitakiwa kusema sasa mgojwa yuko afrika kusini au India,
  Sio tu DC hata mganga wa mkoa walitakiwa kuwajibika.
  Ushauri. Kama polisi inapiga risasi waandishi wa habari ni wazoefu wanamwachaje huyo anayekula watu si sawa na simba mla watu?

  ReplyDelete
 8. kati ya mwndishi wa habari, na mtu mla watu inaonekana kwamba mwandishi ni mtu hatari sana katika jamii kuliko huyu mtu mla watu ,ndo maana kwake sheria inachukua mkondo wake ilhali risai na mmabomu hutumika kwa waandishi wa habari.hii ndo TANZANIA nchi yangu na kisiwa cha amani.!

  ReplyDelete
 9. God Please Help us....tunakoelekea nipabaya...hiyo appetit ya kula ulimi wa mbwa na mtu reception yake...makubwa

  ReplyDelete
 10. huyo jamaa inawezekana anatumia nguvu za giza au ni masharti ambayo amepewa na mganga wake wa kienyeji ili kupata kitu alichoomba kwa magagula hao.Tumetoka kwenye viungo vya albino sasa tunakwenda kwenye kula nyama za mbwa na watu.Watanzania tukae chonjo katika dunia hii usimwamini mtu yeyote hata ndugu yako.

  ReplyDelete