18 September 2013

TBS YAFUNGA KIWANDA CHA UZALISHAJI NONDONaMwandishi Wetu, Kib aha
SHIRIKA la ViwangoTanzania (TBS) limesitisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha nondo cha Hong Yu Steels COT LTD kilichopo Visiga wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani hadi pale kitakapo kamilisha taratibu za kuwa na leseni za ubora wa viwango
.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusitisha shughuli za kiwanda hicho,mkaguzi wa viwango vya vyuma wa TBS,Yona Afrika ,alisema kuwa baada ya kufanya ukaguzi waligundua kwamba nondo zinazozalishwa katika kiwanda hicho hazina viwango upande wa ukubwa.
Alisema kuwa nondo hizo zina viashiria vya upungufu wa ubora ndiyo maana wameamua kusitisha shughu li za uzalishaji hadi pale watakaporidhika baada ya kiwanda hicho kuthibitisha ubora wa nondo hizo kwa shirika hilo.
Alisema pia wamesitisha nondo zilizokwisha tengenezwa zisitoke nje ya kiwanda hicho hadi pale zitaka pothibitika kwamba ubora wake unaridhisha. Nondo hizo ni zile zenye uzito wa tani255 zenye unene wa mita 12 na tani 14 zenye ujazo wa mita14.Alisema kuwa pia TBS itatoa muda kwa uongozi wa kiwanda hicho kurudisha nondo zilizokwishapelekwa kwa wateja .
Alisema ni rahisi nondo hizo kurudishwa kwa kuwa zina jina la kiwanda hicho. Naye,Mwanasheria waTBS, Baptista Bitaho,alisema shirika hilo linafanya kazi kupitia sheria namba mbili y aviwango ya mwaka 2009 na kwa kupitia sheria hiyo linafuatilia wadau wake ili kuhakikisha wazalishaji wanakuwa na leseni za ubora.
Alisema kuwa pale wanapoona mzalishaji anakwenda kinyume na kukiuka sheria za viwango TBS inachuk ua hatua kw akusimamisha uzalishaji kwa muda hadi pale mzalishaji huyo atakapofuata sheria za uzalishaji.
Alisema katika kutekeleza azma ya shirika hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi kub wa ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kupokea rushwa.
Mkalimani wa wamiliki wa kiwanda hicho ambao ni raia wa nchini ,Ernest Sinje,alisema TBS kusitisha uzalishaji wa kiwanda hicho ni hujuma kutoka kwa viwanda vingine vinavyotengeneza nondo nchini.
Alisema kiwanda hicho ndicho kinazalisha nondo zenye ubora kwa Tanzania

No comments:

Post a Comment