Na
Reuben Kagaruki
MAMLAKA ya
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), i m e a m u r u kusimamishwa mara
moja kwa mpango wa tozo ya ufuatiliaji mizigo bandarini kwa njia ya mtandao
(Electonic Cargo Tracking Note-ECTN) uliopigiwa debe na Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA).
Hatua hiyo ya SUMATRA inatokana na malalamiko ya Chama Cha Mawakala wa
Meli Tanzania (TASAA) kupinga mpango huo na kumwandikia Mkurugenzi Mkuu wa TPA
kutaka mpango huo usitishwe.Mpango huo ulipangwa kuanza
kutumika kwa mizigo yote inayoingia bandarini kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Pamoja na kulalamikia dosari m balimbali zilizojitokeza kwenye mpango huo likiwemo suala la
kutoshirikishwa wadau katika mjadala wa wazi kwa mujibu wa SUMATRA, TASAA iliukataa
mpango huo kwa maelezo kwamba ni batili na haupaswi kutumika kwa kuwa uliwaweka
kando wadau na unaongeza gharama zisizo za lazima.
Barua ya TASAA yenye kumb.
HS /TASAA/TPA/ 130712 ya Julai 12, mwaka huu iliyotumwa kwa Mkurugenzi wa TPA,
ilielezea wasiwasi wa wadau kuhusu matokeo ya kiuchumi yanayoweza kuikumba
sekta hiyo na taifa kwa ujumla endapo mpango huo ungetekelezwa.Barua hiyo iliyosainiwa na
Katibu wa TASAA, Peter Kirigini, iliwataka wateja wa chama hicho kote duniani
kupuuza waraka huo wa TPA kutangaza matumizi ya ECTN, sambamba na kuitaka
mamlaka husika SUMATRA kuingilia kati mara moja suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.
Baada ya SUMATRA kupitia
suala hilo,
ilifikia mwafaka na kutoa maamuzi kusitisha mara moja mpango huo. Katika hukumu
yake iliyosainiwa na Mkurugenzi wake, Kilima, SUMATRA
imejiridhisha kwamba ni kweli TPA ilisaini makubaliano ya kuanzisha mpango huo
na ulipangwa kuanza kutumika Septemba mosi 2013 kwa mizigo yote ya meli
inayoingizwa nchini.
Katika uamuzi wake SUMATRA imeeleza kuwa tayari kuna mifumo (systems)
inayotumika kufuatilia mizigo kuanzia inapopakiwa na pia kuna mifumo inayofanya
kazi vizuri kupima thamani kwa CIF.Pia SUMATRA ilibaini kwamba
TPA haikushirikisha wadau wakubwa wa bandari katika uanzishwaji wa mpango huo
na kueleza kwamba matumizi ya ECTN yataongeza gharama kwa mawakala wa meli na
mzigo huo utawaangukia wanaoingiza bidhaa moja kwa moja na hatimaye kuwagusa
watumiaji wa mwisho.
SUMATRA
imebainisha kwamba matumizi ya ECTN yataongeza mchakato na mlolongo wa nyaraka
hivyo kusababisha gharama zingine kwa mawakala wa meli na kuweka wazi kwamba,
mbaya zaidi bandari zingine shindani hazijaona umuhimu wa matumizi ya mpango
huo, hivyo matumizi ya ECTN utasababisha mdororo kwa bandari zetu.
P i a i m e s e m a k w a
kutegemea huduma za kampuni ANTASER BVBA itasababisha shughuli za kuingiza
mizigo kuwa za kificho jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi kwa kukosa
usimamizi wa mizigo inayoingia.Kutokana na mazingira hayo, SUMATRA
imeitaka TPA kuiagiza Antaser BVBA kuachana na mpango wake wa kuanzisha ECTN
sambamba na kuondoa jedwali la gharama lililokwishawekwa kwenye mtandao wake.
SUMATRA
imeitaka TPA kuiagiza Antaser BVBA kutumia mtandao wake kuwafahamisha mawakala wa
meli kwamba utekelezaji wa matumizi ya ECTN umesitishwa na kwamba TPA ilipaswa
kuwasiliana na mdhibiti kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo kabla ya
kuanzisha huduma ya ECTN.TPA ambao waliingia mkataba na kampuni
moja ya Ubelgiji, iitwayo ANTASER BVBA kwa lengo la kuanzisha tozo hiyo.
Tozo hiyo ya ECTN ilikuwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa mzigo
kutoka nchi inakotoka kwa njia ya mtandao, kazi ambayo wadau walisema hufanywa
na kampuni za meli na zile za wakala wanaosafirisha mizigo hiyo na si dhamana ya
TPA ambao jukumu lao ni kupokea mizigo kutoka kwenye meli cargo handling) na
kuhifadhi kwa muda ikisubiri wateja kuichukua
No comments:
Post a Comment