ZAIDI ya sh.milioni35 zimetumika kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kwa ajili ya kuendeleza biashara zao, anaripoti Re hemaM aigala.
Akizungumza katika mafunzo
ya ujasiriamali juzi jijini Dar es Salaam,Ofisa Mikopo wa Taasisi ya Inuk
a Wanawake na Maendeleo, David Msuya alisema tayari wameshakopesha pesa hizo kwa
wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuwa,katika
Mkoa wa Dar es Salaam tayari wanachama 29,000 ambao wengi wao wamesha kopeshwa mkopo
mdogo ambao hauna riba unaoanzia sh. 30,000.
Hata hivyo, alisema hivi
karibuni wamepata wajasiriamali wapya 30 wanaotoka Mbezi Mpigi Magoe, Wilaya ya
Kinondoni ambapo tayari wameshawakopesha sh. milioni 1.8.
Vile vile, Msuya alisema hivi sasa wana vituo 16
ambavyo vipo Dar es Salaam, Shinyanga, Tanga, Tunduru, Lindi na Mtwara.Hata hivyo, ofisa mikopo huyo aliwataka
wajasilimari kuwa wa kweli katika biashara zao na kuwa wabunifu.
“Mjasiriamali yeyote anatakiwa kuwa mbunifu wa
kujua leo atengeneze nini ili aweze kupata wateja wengi kushinda mwenzake na si
kuigizana bidhaa,” alisema Msuya.Hata hivyo, taasisi hiyo ilisema lengo lake ni
kuinua wajasiriamali wa chini ili waweze kuwa wakubwa
No comments:
Post a Comment