03 September 2013

SIKUAPA KUITETEA CHADEMA-BAREGU

  • ADAI KUIGOMEA KAMATI KUU,CCM YAMPONGEZA

 Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ame s ema b a a d a y a kuteuliwa kwenye nafasi ya ujumbe wa tume hiyo, alikula kiapo cha kutetea masilahi ya Watanzania si ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Prof. Baregu aliyasema hayo juzi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia jijini Mbeya wakati akifungua Baraza la Katiba jijini humo na kuongeza kuwa, huo ndio mwanzo wa mgogoro uliokuwepo kati yake na viongozi wa CHADEMA.

"Wote mliofika katika baraza hili, mmeheshimiwa sana na Watanzania wenzenu waliowatuma mbebe mawazo yao ili yawekwe kwenye Katiba Mpya ambayo itadumu zaidi yamiaka 100...nawaomba msitetee masilahi ya vyama vyenu bali ya Taifa," alisema Prof. Baregu.Aliongeza kuwa, mbali ya kuwa mjumbe katika tume hiyo pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA ambapo wakati fulani kulikuwa na sintofahamu kati yake na viongozi wake.

Alisema CHADEMA walimtaka afike kwenye Kamati Kuu lakini aliwagomea kwa sababu alitambua alichokuwa akikifanya, kilikuwa kwa manufaa ya Watanzania si chama chake."Mimi s i k u a p a k u i t e t e a CHADEMA hata kama ni kada wake bali niliapa kuitetea Tanzania na wananachi wake, vyama vya siasa vinaweza kufa lakini Tanzania haiwezi, itaendelea kuwepo milele hivyo lazima tuheshimu hilo," alisema.

Prof. Baregu alisema kwa kutambua umuhimu wa vyama vya siasa kupewa nafasi na tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba, ilitoa nafasi kwa vyama hivyo kuunda Mabaraza ya Katiba, kukusanya maoni yao na kuyapeleta kwenye tume.Alisema fursa hiyo ndiyo inayoweza kutumiwa na vyama hivyo kutetea masilahi ya vyama si kwenye mabaraza ya wananchi.

"Vyama vya siasa vina nafasi yao ya kuunda Mabaraza ya Katiba na kujadili kwa mfumo ambao wataona unafaa, haya mabaraza tuwaachie wawakilishi wa wananchi ambao ndio ninyi."Hata katika tume, kuna wakati tulikuwa tukitofautiana mawazo lakini tunafikia muafaka kwa mfano, mimi ni muumini wa Serikali moja lakini nimewaletea rasimu yenye Serikali tatu," alisema.

Maelezo hayo ya Prof. Baregu, yaliwafanya wajumbe waliotoka CCM katika mabaraza hayo, kumpongeza kwa busara zake za kutanguliza uzalendo na masilahi yaTaifa.C HADEMA kilitangaza kujitoa ka tikamcha katow a mabadi liko yakati ba nakuda imchakatohuoumetekw an aCC Mnakudai wajumbew atu mehiy o h awanaweledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

Kuto kana nahalihiyo, cha mahichokilidai h akir idhishwina mchak atom zima wakut ungaKatibaMp ahivyok ilim takaProf. Baregu ajitokekw enyetum eili chamakianzis hekamp eninc hinzima ya kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo.

5 comments:

  1. Wewe ni profesa hasa, maana wengine ni maprofesa lkn wagumu kuelewa, nakupongeza profesa

    ReplyDelete
  2. Tungeweka uzalendo mbele km prof wetu huyu, hata hizi fujo za kitoto bungeni zisingekuwepo. Taf prof endelea kutoa somo. NAKUpONGEZA SANA

    ReplyDelete
  3. Napenda sana waliosoma na kuelimika ingawa mimi siyo msomi,Taifa lingekuwa na 10% tu ya watu kama huyo Pro.hakika tungekuwa mbali,wastaarabu hata siku moja hawana maamuzi ya nguvu kufikia suluhu la jambo.Hongera Pro.

    ReplyDelete
  4. Kwanza next time mwandishi awe makini kuandika mtandaoni haswa swala la spelings. hii story not edited kabla ya published, hapo mwisho haieleweki but prof. anafanya kazi nzuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hongera prof. Bunge limepwaya kutokana na kuingia watu wasio wanasiasa bungeni. Wangine ni mabongo fleva na wengine hawana ajira hivyo wamejipatia ajira. Wanaipalilia kwa kucheza na bongo za watu (Brain washing)

      Delete