18 September 2013

SERIKALI KUENDELEA KURAHISISHA MIFUMO UOMBAJI MIKOPO



 Na Rehema Mohamed
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt.Florens Turuka,amesema maboresho yaliyokwishafanyi ka ya usajili wa rasilimali na mali mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kuombea mikopo benki y ataendelea kufanyika ikiwa ni juhudi za kupambana na umaskini
.Turuka alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi. Alisema kuw a serikali imefanya maboresho hayo ili kuzidi kuvutia biashara na uwekezaji.“Kipindi cha nyuma ilikuwa inachukua wiki mbili hadi tatu kusajili rasilimali na mali,lakini kwa sas a inachukua siku tano tu,”alisema na kuongeza kuwa lengo ni kufanya watu waweze kuwa na dhamana ku ombea mikopo benki.
Alisema pamoja na Serikali kufanya maboresho hayo, bado kuna tatizo la watu kutumia dhamana moja kuomba mkopo kwenye benki zaidi ya moja .Alisisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kufanya hivyo ni kosa kubwa. Alifafanua kuwa utar atibu wa kutumia dhamana moja kwa ajili ya kupata mkopo ni waki mataifa.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imeamua kuweka mifumo madhubuti kudhibiti hali hiyo,” al isema.Alifafanua kwamba benki zina mfumo na utaratibu wa kubadilishana taarifa ambao unasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). “Serikali imeweka mfumo mzuri wa kubadilishana taarifa ambapo tayari kumewekwa kanuni zinazosima miwa na BoT,”alisema.
Alisema jukumu  la benki hiyo kuu ni kukusanya taarifa mbalimbali, kusimamia na kusam baza katika mabenki hapa nchini .“Lengo la kufanya hiyo ni kuzuia watu kukopa kwenye benki mbili tofauti kwa dhamana moja.hiyo husaba bisha riba kuwa kubwa sababu benki zina wasiwasi wa kupata hasara,”alieleza.
Aidha alisema shughuli za ujenzi wa  barabara , madaraja na majengo makubwa zinazoendelea, zinaonesha uchumi wa Tanzania umeimarika kwa kiasi kikubwa.
Aliongeza kusema kuwa huu ni wakati kwa sekta binafsi kutumia fursa zilizopo kufanya biashara na uw ekezaji kwa ajili ya kukuza uchumi.“Tunahitaji kuona sekta binafsi inaongeza uzalishaji ili kuweza kuuza zaidi bidhaa za Tanzania nje ya nchi,” alisema

No comments:

Post a Comment