11 September 2013

'SERIKALI IELEZE ZILIPO FEDHA ZA DECI'



 Na Rehema Maigala
MBUNGE wa Ubungo, J o h n Mn y i k a , amemtaka Gavana wa Benki Kuu (BoT), Benno Ndulu, kuwaeleza Wa t a n z a n i a , h u s u s a n waliokuwa wanachama wa Kampuni ya Development En t e r p r e n e u r s h i p f o r Community Initiative (DECI) fedha zao zipo kwenye akaunti gani.

Mnyika amesema kuwa wakati sakata la DECI linaanza mwaka 2009, Serikali ilizuia akaunti ya DECI iliyokuwa na sh.bilioni 19, sawa na asilimia 40 ya fedha zote ambazo ni za wanachama wa taasisi hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara juzi, Kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza, baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wananchi aliyetaka kujua hatima ya fedha zao, Mnyika alitoa tahadhari kuwa dana dana inayotaka kufanywa na Serikali kuwalipa watu hao kiasi cha sh.bilioni 19, inaweza kutia shaka kuwa fedha hizo hazipo.
"Sasa naomba nimjibu yule mwananchi aliyetaka kujua hatima ya fedha za DECI...mtakumbuka hili suala nimekuwa nikitaka majibu yake bungeni, lakini kila mara wanatumia kisingizio kuwa suala hili liko mahakamani. Juzi baada ya hukumu kutoka tumemsikia Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, akisema hawawezi kuwalipa wananchi walioweka fedha zao DECI.
"Wanasema waliocheza DECI nao ni watuhumiwa, walipaswa kuhukumiwa, lakini Gavana hakusema hizo fedha sh.bilioni 19 sawa na asilimia 40, ambazo Serikali ilizitaifisha na kuwekwa BoT, ziko kwenye akaunti gani, tunataka atuambie, maana kwa hali inavyoanza isijekuwa fedha hizo walizitumia kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.
Mbunge huyo alisema kuwa wananchi waliopanda fedha zao wana haki ya kulipwa kwa sababu zipo zikishikiliwa kwenye akaunti na Serikali. Zinapaswa kurejeshwa kwa msingi kwamba pamoja na mahakama kuwahukumu waendeshaji wa DECI kuwa ni wahalifu, haikuwahukumu washiriki.
Aliongeza kuwa DECI ilisajiliwa na Serikali na viongozi wa Serikali, akiwemo Waziri wa Fedha na Uchumi wa wakati huo, Mustafa Mkulo, walihamasisha watu kujiunga. Serikali iliachia kuendeshwa na kuzilinda ofisi za kampuni hiyo maeneo ya Mabibo, ambapo ni jimboni kwa mbunge huyo.  

1 comment:

  1. IWAPO SHUGHULI HII HAIKUWA HALALI WOTE WALIOIFANYA WANAHESABIWA KAMA WAHALIFU KAMA MTU ANATAKA KUISAIDIA SERIKALI KWA KUJITAJA KUWA NAYE NI MHALIFU SI AJISALIMISHE POLISI TATIZO LA WATANZANIA WANAPENDA FEDHA BILA KUTOA JASHO NA WENGI KUDAI HAKI MSAMIATI WA WAJIBU KWAO HAUPO MUNGEMCHAGUA MZEE CHEYO AWAJAZE MAPESA MFUKONI ILA IMEANDIKWA KWA JASHO UTAKULA BURE GHARAMA

    ReplyDelete