Na Mwandishi Maalumu
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema
Serikali itahakikisha kuwa ardhi ambayo Watanzania wamepewa na Mungu
haibadiliki na kuwa chanzo cha upotevu wa amani nchini.Kauli hiyo
aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Kimataifa wa siku
tatu unaojadili haki na amani katika masuala ya ardhi Tanzania.
"Tutafanya
kila tuwezalo kuhakikisha kuwa ardhi yetu haileti laana, bali inabakia kuwa
baraka ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia. Ninawasihi wale wote wenye mamlaka na
utoaji wa ardhi wahakikishe kuwa wanatimiza wajibu wao wanaposimamia masuala ya
ardhi ili haki isipotee na hatimaye kuepusha migogoro ya ardhi.
"Ninawasihi
Watanzania iwe ni wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia, wasomi na umma
wote kwa ujumla. Ninaomba tuitunze amani tuliyonayo na tutambue kwamba Tanzania
ndiyo nchi pekee tuliyojaliwa kuwa nayo. Madhara ya ukosefu wa amani ni
makubwa, tuangalie nchi za wenzetu zenye migogoro na tuone jinsi machafuko hayo
yatatuathiri sisi wenyewe, watoto wetu na wajukuu wetu," alisisitiza
Waziri Mkuu.
Alisema, anatambua
hofu ambayo imewakumba watu wengi kuhusiana na uwekezaji iwe ni kwenye kilimo
ama madini."Ninatambua
kwamba kuna hofu kubwa imejengeka miongoni mwa wananchi wengi hasa wanaposikia
suala la uwekezaji hasa kwenye kilimo," alisema. Alisema, tangu wakati
wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa madarakani, alishasema
kuwa ardhi ni rasilimali ya watu wote.
"Aliweka mifumo
ambayo hairuhusu mtu kumiliki ardhi ambayo haina ukomo, kuna ukomo wa miaka
kati ya 33 na 99. Na pia kuliwekwa masharti kuwa ni lazima ukipata ardhi
uiendeleze, usipoiendeleza, unanyang'anywa," aliongeza.
Alisema, kwa mujibu
wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, imekataza mgeni (mtu ambaye si raia wa
Tanzania) kumiliki ardhi hapa nchini." A r d h i i n
a t o l e w a k w a wawekezaji, chini ya sheria ya uwekezaji kwa muda maalumu.
Mwekezaji akimaliza muda wake, anatuachia ardhi yetu na ndiyo maana Serikali ya
Kijiji hairuhusiwi kutoa ardhi zaidi ya ekari 50," alisema.
Alisema, chini ya
sheria ya ardhi na sheria ya uwekezaji, hapa nchini kuna wawekezaji wakubwa 122
ambao ni wa ndani na wa nje na kwa ujumla wao wanamiliki kilomita za mraba
1,296 kati ya kilomita za mraba 945,087 ambazo ni ukubwa wa nchi nzima.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 200 wakiwemo Rais mstaafu, Benjamin
Mkapa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka,
wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, viongozi wa dini, washiriki kutoka nchi za Ujerumani, Sweden,
Burma, Finland, Norway na Afrika Kusin
No comments:
Post a Comment