Na Fatuma Rashid
Timu ya Mtibwa Sugar imedhamiria kuondoa
mdudu wa sare anayeiandama timu hiyo mara kwa mara.Akizungumza kwa simu akiwa Morogoro
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Salum Kijazi alisema hivi sasa wanajipanga ili waweze
kufanya vizuri katika mechi dhidi ya Ashanti United.
Kijazi alisema katika
mechi, lazima kunakuwa na upungufu mbalimbali ambao husababisha wapinzani
kutumia kama faida, hivyo timu yake inaendelea kurekebisha makosa
yaliyojitokeza.
"Unajua katika kila mechi kuna
upungufu wake na mpinzani wako hutumia kama faida, ila kwa kipindi hiki timu
imejipanga vizuri na imefuta makosa yote ambayo kama tusingeyarekebisha
tungekuwa katika nafasi mbaya," alisema.
Alisema msimu huu kila timu ipo vizuri,
hivyo inasababisha kila mechi wawe wanajiandaa vizuri na kutumia kila mbinu
katika mechi."Katika mpira unapoingia uwanjani
hautakiwi kukurupuka, wachezaji wanatakiwa kujipanga na kujua ni mbinu gani
wanazotumia timu pinzani, ili waweze kupambana nao, hivyo vijana wanajipanga ipasavyo
kwani ligi inazidi kupamba moto kutokana na kila timu kujiandaa vizuri,"
alisema.
Akizungumzia waamuzi wanaochezesha Ligi
Kuu msimu huu, Kijazi alisema katika mechi iliyopita dhidi ya Prisons mwamuzi
alikuwa akifanya makosa hivyo walichukulia kama makosa ya kawaida.
"Waamuzi wote wanachezesha vizuri,
ila kuna makosa y a k i b i n a d amu amb a y o huwa yanatokea kwani huyo
anayechezesha ni binadamu pia hivyo kuna haja ya kukaa na kuongea naye,"
alisema.
Alisema
katika mechi dhidi ya Ashanti
wamejipanga kufanya vizuri, licha ya kuwa na majeruhi ambao ni Mussa Hassan
'Mgosi' na Masudi Ally, walioumia wakati wa mazoezi lakini wanaamini katika
mechi hiyo wataweza kucheza kutokana na hali zao kuwa nzuri.
No comments:
Post a Comment