26 September 2013

'MFUMO WA ELIMU UBORESHWE NCHINI'



 Na Allan Ntana, Tabora
Serikali  kupitia watendaji wake imeshauriwa kuboresha mfumo wa utoaji elimu hapa nchini ili elimu hiyo iweze kumpa msingi mzuri na mwanga utakaomsaidia mwanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yake.Sambamba na hatua za kumuwezesha kufanya vizuri katika kujiendeleza kielimu.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Kanisa la FPCT hapa nchini, Mchungaji David Batenzi katika sherehe za mahafali ya 23 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Umoja iliyoko wilayani Igunga mkoani Tabora.
Sherehe iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikwa na kanisa hilo.
Alisema, serikali inaweza kupitia upya mfumo wake wa elimu na ikiwezekana ikaufanyia marekebisho kwa lengo la kuboresha mtaala unaotumika kwa sasa ili mfumo huo uweze kumsaidia mwanafunzi kupata msingi mzuri kielimu.
" Hatujisik i vizuri tunapoona matokeo mabaya kwa wanafunzi wetu hasa yanaposababishwa na dosari kadhaa za kimfumo kutokana na kubadilishwa mara kwa mara pasipo kufanya utafiti, katika hili viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu hiyo hapa nchini wanapaswa kulaumiwa, mfano matokeo ya kidato cha nne mwaka jana hali ilikuwa tete," alisema askofu

No comments:

Post a Comment