02 September 2013

MCHUNGAJI:MIGOMO IEWPO KWENYE KATIBA Na Yusuph Mussa, Korogwe
MCHUNGAJI wa Kanisa la Anglikana, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Stephen Daffa, amesema Tanzania ya sasa, ili wafanyakazi wasikilizwe na kupata haki zao, lazima wagome au kuandamana; hivyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ikubali kuingiza kipengele hicho kwenye Katiba Mpya.Alisema kipengele hicho kikiwepo, waajiri wataona umuhimu wa kusikiliza na kutatua kero za wafanyakazi wao.

Mchungaji Daffa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye Kikao cha Maboresho ya Rasimu ya Katiba Mpya kilichoandaliwa na Asasi ya Tanzania Environment Relatives Organization (TERO) ya Mjini Korogwe kwa ufadhili wa Shirika la The Foundation for Civil Society la Dar es Salaam.
Mkutano huo ulishirikisha wananchi wa Kata za Kerenge na Magoma wilayani humo ambapo akichangia maoni hayo, Bw. Ramadhan Mswaki, alisema badala ya mwalimu au daktari kuchukua uamuzi wa kugoma kwa madai ya kuonewa au kupunjwa mshahara, waandike barua ya kuacha kazi.
Naye Mwalimu Edith Kimea, aliomba Katiba Mpya iwe na kipengele cha kutoa uhuru kwa viongozi wa wafanyakazi ili wasiendelee kutishwa na viongozi wa Serikali unapotokea mgomo ambapo hivi karibuni, Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT), Wilaya ya Korogwe, Fesstus Mitimingi, alikuwa anatafutwa ili awekwe ndani..

No comments:

Post a Comment