02 September 2013

MPANGO WA 'MATOKEO MAKUBWA' WAPINGWANa Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI ya wadau wa elimu wamepinga mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na kudai umezibagua shule binafsi wakati fedha zilizotolewa na wafadhili ikiwemo chenji ya rada ni kwa ajili ya Watanzania wote.

  Wadau hao waliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano Mkuu wa wazazi wenye watoto wanaosoma Shule ya Sekondari Lwandai, iliyopo Mlalo, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.  
 Akiwasilisha taarifa kwa wazazi, Mkuu wa Shule hiyo, Lewis Sameji, alisema walitarajia mpango huo ungelenga kuboresha elimu kwa watoto wote, lakini wanashangaa kuona unazihusu shule za Serikali pekee na kuziacha za binafsi."Hali hii inaonesha Serikali haioni mchango wa sekta, taasisi na asasi binafsi katika kukuza elimu nchini, dhana ya mpango huu inawahusu Watanzania wote si jambo la kisiasa. "Wakati      Serikali inaleta mpango huu kwenye sekta ya elimu ni juu yetu sisi wazazi kutafakari kwa makini kuhusu dhana hii, je, nasi wa shule binafsi tutapewa fursa za kielimu," alihoji Sameji.Alisema wanafunzi wote ni sawa lakini ruzuku kwa shule zinazomilikiwa na taasisi binafsi hakuna ambapo vitabu vilivyonunuliwa kwa fedha ya rada, vilipaswa kugawanywa kwa shule zote bila kujali ya Serikali au binafsi.  
  Aliongeza kuwa, rasilimali ambazo zitawezesha mpango huo ni za Watanzania wote. Alisema changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni ujenzi wa bwalo ambapo marafiki zao Wajerumani wamekubali kuwasaidia kulijenga." H a w a m a r a f i k i z e t u hawatafanikisha ujenzi wote hivyo ni jukumu la wazazi na wadau wengine, kumalizia jiko...ujenzi wa bweni la wasichana umeanza, kwa kiasi kikubwa ukitegemea michango ya wazazi," alisema.
Sameji alisema shule hiyo ambayo inachukua wanafunzi mchanganyiko wavulana na wasichana, ina wanafunzi zaidi ya 600, kompyuta 10 hivyo kushindwa kukidhi haja ya wanafunzi kujifunza pia inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya michezo na viwanja vya kuchezea.

No comments:

Post a Comment