03 September 2013

KILOLO YAVUKA MALENGO YA MAPATO YAKE



 Na Eliasa Ally, Kilolo
HAL MASHAURIya WilayayaKilolo iliyop omkoani Iringakwamud awamiezi mitatu ime wezak uku sanyamapato ya ndanish. 295 ,144,378.33kutokakwenye v yanzombalimbali vyamap atoyak eyand an i nakufikia asili mia97 yale ng olakuk usanyamapato.

Akizungumza jana wakati akitoa taa rifayau teke lezaji wash ughuli zaseri kal ikwakipindi c hamieziminneofi sinikwake, M kuuwaWilaya yaKilo lo, GeraldGuni nita alisema kuwa wilaya hiy oiliku waimejiwekeamalengoh ayona kuvukaasili mia60 .
Alise makuw amapato hayo yameanza kukusanywa kuanzia mwezi Mei hadi Agosti mwaka huu ambapo mapato hayo yanatokana na vyanzo vya ndani yakiwemo mbao, mazao ya kilimo, mifugo, biashara ndogondogo na kubwa ndani ya wilaya hiyo.
Guninita alisema kuwa katika mwezi wa Julai, Wilaya ya Kilolo iliweza kukusanya jumla ya sh.69,014,520 sawa na asilimia 60 kwa mwezi huo pekee ambapo fedha hizo zilikuwa zimetumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali za wilaya na miradi kupitia idara zake zilizomo wilayani humo za ujenzi, elimu, barabara, maji, afya, kilimo, umeme, mawasiliano na misitu.
Alisema kuwa katika idara ya ujenzi wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali ambapo baadhi ya shughuli hizo zimekamilika ambapo jumla ya sh. 1,729,481,900 zimetumika na miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kuanzia kipindi cha mwezi Mei 2013 hadi Agosti 2013 na kuwa baadhi ya kazi hizo zimekamilika.
Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefanyiwa matengenezo ya kawaida na ya kudumu katika barabara kuwa ni jumla ya kilomita 54 ambapo kutoka Idete kwenda Kiwalamo hadi Kimara kilomita 16 zimetumia sh. 189,960,000, barabara ya Makungu hadi Mlafu kilomita 6 imegharimu sh.mil 86,barabara ya kutoka Ihimbo kwenda Kitelewasi kilomita 20 imegharimu sh. milioni 285, barabara ya Ruaha Mbuyuni kwenda Msosa kilomita 7 imegharimu sh.53,607,000 ambapo barabara ya kutoka Ukumbi kwenda Pomerini kilomita 5 imegharimu sh.milioni 20.
“Ujenzi wa madaraja mawili na vivuko vya barabara ya Idete, Kimara hadi Kiwalamo tumejenga madaraja makubwa mawili na makaravati kwa sh. 153,130,000 ambapo daraja la Kiwalamo pekee limegharimu gharama ya sh. milioni 108 na tunashukuru kazi hizo zimeweza kukamilika kwa muda mwafaka ambao ulipangwa na kukubaliana na wakandarasi na kuzikamilisha”, alisema Guninita

No comments:

Post a Comment