03 September 2013

BODI YA KOROSHO YATANGAZA BEI ELEKEZIBODI yaKo roshoTanzania imet ang azabei e lekezi yakoro sho k uwanish .800kw akilokwakoro sh od araj ala kw anz anakorosho da rajalap ili ni sh600k wa msimuw amwa ka 2013hadi2014, anaripoti Mwandishi Wetu
.Beih iyoi litangazw a ju zi kwenye kikao cha wadauwakoroshokilichofa nyika sikumbil i Mjini Dodomakwakujum ishawadauwotehapa nch ini.Ak itangazabeihiyo Mkurugenzi wa Bodi, Mfaume Juma, alisema kuwa soko la korosho nchini India halijatulia hivyo bei ya korosho nchini India kwa kilo ni sh.1070 ambapo kwa mujibu wa utafiti kuhusiana na gharama za korosho imefikia sh. 724.
Mfaume aliwataka wakulima wa korosho kuelewa kwamba bodi hiyo imeweka bei hiyo ndogo ili kuwavutia wanunuzi kuliko bei kubwa ambayo haina tija.Alitolea mfano nchi za Magharibi kama Ivory Coast na Senegal kwamba ni wakulima wakubwa wa korosho Barani Afrika lakini wanauza korosho kwa bei ya chini inayofanya hawawi na matatizo.
Aidha alisema kuwa ni vyema korosho zikabanguliwa hapa nchini ili kuondokana na dhana ya uuzaji wa korosho ghali, ambapo aliongeza kuwa soko kubwa la korosho ni nchini India ambapo zinabanguliwa kabisa na kwenda kuuza nchi nyingine.
Alisema kuwa Vietnam ni wafanyabiashara wa korosho lakini wanategemea sana korosho kutoka nchi za Afrika Magharibi na zinapomalizika ndipo wananunua korosho za Tanzania.Kwa upande wao wadau wa korosho hawakuridhika na bei na kwamba bei haiendani na gharama na kwamba utafiti uliofanywa haukuzingatia gharama za uendeshaji za wakulima.
Akichangia mada Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bi. Hawa Ghasia, alisema mfano takwimu zilizotolewa si sahihi na kuiomba bodi hiyo ikae na kufanya utafiti upya kwa kuwashirikisha wakulima.
Katika mkutano huo wadau wengi walionesha kutoridhika na bei ukizingatia kwamba ushauri uliotolewa wa kukusanya korosho na kupelekwa ghalani kwa ajili ya kusubiri mnada ili walipwe fedha ni kutafuta migogoro kwa wakulimaAidha wadau hao waliomba kuendelea na mfumo wa stakabadhi ghalani lakini walipwe kwanza tofauti na sasa ambapo wakulima wanalipwa sh. 600 halafu baadaye wanamaliziwa sh.200

No comments:

Post a Comment