NAIROBI, Kenya
Serikali ya Kenya,
imesema nchi hiyo ipo katika vita na wapiganaji wa jihadi kutoka nchini Somalia
Al Shabaab.Pia Serikali
nchini humo imekanusha taarifa zinazodai k uwe p o kwa s h amb u l i o
linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab katika jengo la kibiashara la Westgate,
Septemba 21 mwaka huu, zilipuuzwa
. Kwa mujibu wa
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), watu 67 walipoteza maisha katika
shambulio hilo ambalo lilidumu kwa siku nne
ndani ya jengo hilo.Juzi usiku,
Wakenya na raia wa nchi nyingine waliopoteza ndugu zao katika shambulio hilo, waliwasha mishumaa nje ya jengo hilo ili kuwakumbuka waliokufa.
Magazeti ya Kenya yalidai Idara ya Usalama nchini humo
ilitoa ilani mwaka mmoja uliopita juu ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa
Al Shabaab, kupanga kufanya mashambulizi Mjini Nairobi na Mombasa.
Inadaiwa watu hao walipanga kufanya
mashambulizi ya kujitoa mhanga na kulishambulia jengo hilo.
Kamati ya Ulinzi ya Bunge nchini humo,
inakutana leo kuliangalia suala hilo
na ilani iliyotolewa. Ofisa mmoja mwandamizi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani nchini humo, alisema Serikali imekuwa ikipata taarifa kama hizo kila siku.
Aliongeza
k uwa , hatua zimekuwa zikichukuliwa kuepusha mashambulio mengi ambapo Kenya iko vitani na kila siku kijana wa Kenya anashawishiwa
na Al Shabaab kuua Wakenya.
No comments:
Post a Comment