16 September 2013

KATIBA MPYA YAIBUA MAZITO



  • CHADEMA,CUF,NCCR WAMHADHARISHA JK
  • WAMUONYA ASITHUBUTU KUSAINI MSWADA WAKE

 Na Anneth Kagenda
USHIRIKIANO wa vyama vya Upinzani nchini, umemtaka Rais Jakaya Kikwete, asithubutu kusaini Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge mjini Dodoma hivi karibuni
.Tamko hilo limetolewa Dar es Salaam jana na wenyeviti wa vyama vinavyounda ushirikiano huo ambao ni Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), Bw. James Mbatia wa Chama cha NCCR-Mageuzi na Bw. Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Katika tamko lao kwa waandishi wa habari, wenyeviti hao walisema kama Rais Kikwete ataridhia na kusaini mswada huo, nchi inaweza kutumbukia mahali pabaya.Wa l i s ema mswa d a h u o unapaswa kurejeshwa bungeni uweze kufanyiwa marekebisho kwa masilahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla ili iweze kupatikana katiba bora.
Akisoma tamko hilo kwa niaba ya wenzake, Prof. Lipumba alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na mchakato unaoendelea ili kupata Katiba Mpya kuhodhiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kiliupitisha mswada huo bungeni Mjini Dodoma.
"Mchakato wa mabadiliko ya katiba unahitaji uvumilivu, hekima, kuheshimiana, usitawaliwe na ubabe, kejeli kutoka kwa watawala, tukiendelea kufanya hivyo, mwisho wa siku Taifa letu litaingia katika migogoro na machafuko."Katiba ya nchi ni mali ya wananchi si ya CCM, CHADEMA wala NCCR Mageuzi hivyo
 mc h a k a t o wa k e h a u p a swi kuhodhiwa na chama chochote cha siasa, taasisi, makundi ya watu bali misingi ya maridhiano inahitajika," alisema Prof. Lipumba.Aliongeza kuwa, mswada huo ulipitishwa Septemba 6 mwaka huu na yaliyojiri bungeni kabla na baada ya kupitishwa mswada huo, yameufanya mchakato huo kuwa na mashaka makubwa juu ya mustakabali wa nchi.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa Rasimu ambayo ilitokana na maoni ya wadau, taasisi, asasi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana lakini CCM iliweka msimamo wa kupinga mambo muhimu yaliyopendekezwa hususan mfumo wa Serikali tatu.
P r o f . Li p umb a a l i s ema , kinachofanywa na CCM ni kukwamisha mchakato huo na kuhakikisha makundi na taasisi mbalimbali hazipati fursa ya kushiriki kwenye Bunge la Katiba.Hali hiyo inatokana na wabunge wa CCM kutoa mwanya kwa kiongozi wa nchi (Rais), kuwa na mamlaka makubwa ya kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka katika makundi na taasisi.
"Marekebisho hayo yamefanyika kinyume na maoni ya wadau na makubaliano ya awali kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kupokea maoni ya wadau wa Tanzania Bara kamati haikukutana na wadau wa Zanzibar wala wawakilishi wa wananchi upande wa pili wa Muungano," alisema.
Akizungumzia kilichotokea bungeni Septemba 4 hadi 6 mwaka huu, yanayoendelea kusemwa, kutendwa na CCM pamoja na Serikali, alisema ni matokeo ya mikakati iliyowekwa na chama tawala kuhakikisha mswada huo unazingatia masilahi yao.
"Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yetu, tunapaswa kuunganisha nguvu zetu ili kuunusuru mchakato huu ambao hivi sasa umetekwa na CCM pamoja na Serikali yake."Upinzani bungeni walisisitiza Zanzibar haikushirikishwa kikamilifu kuandaa mswada huu, Mei mwaka huu Serikali ya Muungano iliupeleka visiwani humo ukiwa na vifungu sita.
"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), iliujadili na kutoa mapendekezo yao lakini mswada uliopelekwa bungeni uliongezwa vifungu vingi ambavyo havikuwemo katika rasimu," alisema.
Alisema baadhi ya vifungu vilivyoongezwa ni pamoja na kifungu namba 37 kinachohusu kuvunjwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambacho kimerekebishwa bila mashauriano na SMZ.
"Mswada uliopitishwa, unasema tume hii itavunjwa baada ya rasimu kuwasilishwa katika Bunge la Katiba jambo ambalo SMZ hawalijui wanachojua itavunjwa baada ya matokeo ya kura ya maoni."Pia tunalaani ukiukwaji wa Kanuni za Bunge, mila na desturi za kibunge uliofanywa kwa kuingiza vifungu vipya kinyemela, kukiuka masharti ya kushughulikia madai ya taarifa za uongo zilizotolewa bungeni na wabunge wa upinzani kunyanyaswa," alisema.
Prof.Lipum ba alis emakuwa, Septemb a 21,mwakahuu, vyamahivyovina taraji akufanya mkutano mkub wawap amojaambaoutaf any ikaViwa njavy aJ angwani, DaresSal aamikiw an imwanzowahatuaya kuwaeleza jambo hilo wa nanchi .
Kwa up andewake,Bw. MbatiaalisemaRais Kikw etendiye mwe nye uwezow akuivu shakatiba hiyokwani lip on daniya u wezowakehivyo a siogope kuchukuauamuz i huoi likulindam asilahi ya nchinaWat anzania.
Na ye Bw.Mbowealisema, CCM haip asw ikuvu ru gamc hakatohuonasi vitayach a matawala na upinzani bali wahusika ni Watanzania.

1 comment:

  1. Wanasiasa na wanaharakati tu ndio wanaelewa wanachokifanya. Hakuna nguvu ya umma wala mslahi ya wananchi hapa.

    ReplyDelete