16 September 2013

TINDIKALI Z'BAR, POLISI WACHARUKA Na Eckland Mwaffisi

SIKU mbili baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Joseph Mwang'amba kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamik a, Jeshi la Polisi li metoa tamko la kuwasaka wahusika usiku na mchana.


Padri Mwang'amba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, akipatiwa matibabu, alipatwa na tukio hilo mwishoni mwa wiki wakati akitoka kwenye duka linalotoa hu duma ya mawasiliano ya mtandao(intaneti), lililopo eneo la Mlandege,wilayani Ung uja.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso,al isema kutokana na ongezeko la vitendo hivyo, jeshi hilo,Mkemia Mkuu wa Serikali na kikosi Maalumu cha kuzuia uchochezi na ugaidi, wamejipanga kufanya operesheni maalumu.

Operesheni hiyo ni ile ya kuwafuatilia watu wote wanaoingiza , kusambaza na kuuza vimiminika vya tindikali kama wanazingatia sheria zilizowekwa dhidi ya vimiminika hivyo.

"Yeyote ambaye itabainika kwenda kinyume hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na k ufikishwa mahakamani, tutaendelea kuwasaka watu wanaofanya vitendo hivi, tunaomba wananchi wenye taarifa nao, wazitoe na zitakuwa siri,"alisema.

Juzi Padri Mwa ng 'amba alitembelewa hospitali na Rais wa Zanzibar,Dkt.Ali Mohamed Shein na kumwe leza kuwa, miezi mitatu iliyopita alitishiwa kuuawa.Katika tukio lililomkuta mwishoni m wa wiki,Padri Mwang'amba alijeruhiwa usoni, mikononi na kifuani.

No comments:

Post a Comment