11 September 2013

JUKWAA LA KATIBA SASA KUMVAA JK



Na Mariam Mziwanda
JUKWAA la Katiba nchini,linatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kupeleka mapendekezo ya kufutwa maamuzi yaliyofanywa na Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Bw. Deus Kibamba,aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano ulioshirikisha wadau na wataalamu 200 kutoka ndani na nje ya nchi. Mkutano huo ulikua  ukijadili mwelekeo wa  maandalizi ya Katiba Mpya na kuongeza kuwa,wabunge hawakutumwa na wananchi kufanya maamuzi hayo.
Alisema lengo la kumwona Rais Kikwete ni kumtaka asitishe hatua za wabunge na wanasiasa kutokufanya kazi isiyowahusu ili kuepusha vurugu na malumbano ndani ya Bunge.
“Mwelekeo uliopo utasababisha wananchi wakose Katiba waitakayo,kutokamilika kwa wakana Uchaguzi Mkuu 2015 kufanyika bila katiba mpya hali ambayo itazua mgogoro.”Ni hatari kuingia katika uchaguzi tukiwa na Katiba ya zamani….hali hii itasababisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba iongezewe muda jambo ambalo wananchi hawapo tayari,hivyo ni muhimu Rais Kikwete aliangalie,”alisema.
Aliongeza kuwa mchakato huo kwa sasa upo njia panda kwani hakuna mwananchi aliyemtuma mbunge kuingilia kazi ya mchakato wa katiba,bali Bunge limesahau kuwa kazi yao ni kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba na kusimamia bajeti ili wananchi kushiriki na kufanya maamuzi juu ya Katiba waitakayo.
Alisema kupitia kikao chao na Rais Kikwete ,watapendekeza wabunge kabisa kwenye mchakato huo kwani kuna watu waliochoshwa na maisha ya sasa. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Palamagamba Kabudi,alisema watahakikisha maoni ya wananchi ambayo hayapo katika Rasimu ya Katiba,yanawasilishwa kwa Rais Kikwete na kusisitiza kuwa,upatikanaji wa katiba bora unawezekana.

10 comments:

  1. mawazo yenu ni mazuri lakini angalieni epukeni kutumika kisiasa kwa kuwa ni ni wataalamu mnategemewa na jamii .

    ReplyDelete
  2. kimsingi mara kwa mara nimekuwa nikifuatilia misimamo yenu nimekuwa nikipata shaka kutokana na jinsi ambavyo mmeshindwa kujipambanua kuwa ninyi ni wanasiasa ,wanaharakati,wababaishaji au wanasheria ,kwani mmekuwa mikidandia hoja hovyo bila ya kueleweka kuwa kazi yenu ni nini acheni tabia ya kupenda umaarufu wa bei rahisi(cheep popularality) tumieni elimu zenu vema .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumeshajipambanua bwana. Sisi ni chadema "B"

      Delete
  3. nadhani mnaojiita jukwaa la katiba hata katiba yenyewe hamjui, ushauri wa bure nendeni kasomeni hata cheti cha sheria kidogo mtapanua mawazo yenu juu ya kitu mnachokipigania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

      Delete
  4. tunapokwenda wa Tanzaia sasa.....tuombe Mungu tu

    ReplyDelete
  5. Rais Kikwete unatakiwa uwe jasiri kutoa maamuzi magumu , usiogope kulaumiwa na wana CCM kwani wenye nchi ni wananchi wenyewe na nyie viongozi mmepewa dhamana ya kusimamia nchi kwa niaba ya watanzania wote.Katiba isiyokidhi matakwa ya wananchi italeta athari kubwa sana sasa na kwa vizazi vijavyo wakati wewe na mimi hatutakuwepo wakati huo Watanzania wakiteseka kwa ujinga na tamaa ya baadhi ya watu wanaotaka kulinda masilahi yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Laaa wenye nchi ni chadema sio wananchi!!!!! NGO ya akina kiwia, lema, aikael, ndesa nk

      Delete
    2. Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

      Delete
  6. Ni kweli sheria ina upungufu. Tatizo ni jinsi Maoni ya Jaji Warioba yanavytafriwa visivyo.

    Tanzania haiko katika vita. Tanzania haiko kwenye utawala wa kiimla! Tanzania inatoa uhuru mkubwa wa kujieleza na kutoa maoni.
    Jaji warioba ni mtu alyeelimika na kubobea kwa fani yake. Anaelewa wazi kua CCM bado ni chaguo la wengi (Majority party). Muelekeo wowote unaoheshimu demokrasia lazima uheshimu maoni na uchaguzi wa wanaccm.
    Mabadilliko ya dhati ya katiba ni muhimu sana kwa wakati huu. Mifumo ya kiuchumi na taratibu za maisha zimebadilika sana. Kuna maswala mapya ama mtambuka kama umilikaji wa aridhi ambayo ni kiu ya kila Mtanzania bila kujali hali yake. Lazima uwekewe mfumo unaoleweka. Kuna uvumbuzi wa raslimali za madini. Ni swala jipya linaltakiwa kuwekewa utaratibu unaeleweka. Kuna maswala ya ndoa na uraia. Watanzania wanaoa na kuolewa nje ya nchi. Linataka kuwekewa utaratibu. Kuna mabadiliko ya mtindo wa uchumi na uwekezaji. Kuna ongezeko la watu na idadi ya watu waliosoma na kupata elimu nzuri na kutoa ushindani katika ajira kuliko hukon nyuma ambapo waliosoma walikua wachache tu. Nalo linatakiwa kuwekewa utaratibu ili kuwe na fair play. Kuna utitiri wa mambo ya msingi.

    La kushangaza ni kuona jinsi wenzetu wasivyotaka kufuata utaratibu wowote ule na kuingiza utashi wao wa kisiasa.
    Jamani hao wanataka kuingia ikulu? Swali ni je wataturuhusu kuwafuata huko ama watatuacha na matatizo yetu? Speed yao yao ni kali mno na inatisha!

    ReplyDelete