- ZMA YATOA TAMKO ZITO,YAKIRI KUISAJILI
Na Mwajuma
Juma, Zanzibar
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Usafiri wa
Baharini Zanzibar (ZMA), Bw. Abeid Omar Maalim, amesema Zanzibar haipaswi
kulaumiwa kutokana na tukio la kukamatwa kwa meli ambayo ilibeba shehena ya
bangi nchini Italia.
Bw.
Maalim aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar
katika kumbukumbu ya kutimiza miaka miwili tangu kuzama kwa meli ya Mv Spice
Islander.
Alisema meli hiyo
ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Gold
Star, iliyopo kwenye
Visiwa vya Marshal, Amerika ya Kusini ilisajiliwa Zanzibar mwaka 2011 ambapo
usajili huo hauna maana kuwa Zanzibar inahusika na tukio hilo.
"Kweli meli hii
ilisajiliwa Zanzibar, jambo la msingi ni kuangalia bangi iliyokamatwa ilipakiwa
wapi na nani anahusika na biashara hiyo," alisema Bw. Maalim.
Aliongeza kuwa, kama
itabainika mmiliki wa meli hiyo anahusika moja kwa moja na usafirishaji huo,
ZMA haitasita kuchukua hatua za kufuta usajili na kuangalia sheria nyingine.
"Kwa mujibu wa
sheria za usajili wa meli, kuna kipengele ambacho mmiliki anajifunga kwa kusema
meli yake haitasafirisha biashara haramu ikiwemo ya dawa za kulevya, ikibainika
kafanya hivyo meli yake itafutiwa usajili," alisema.
NI KWELI NI KUKURUPUKA KUILAUMU ZENJI KWA KUKAMATWA KWA MELI HIYO, MELI NYINGI ZA NCHI MBALI MBALI HUKAMATWA NA MIZIGO HARAMU LAKINI MUHIMU NI MZIGO WA NANI SI MELI IMESAJILIWA WAPI
ReplyDeleteTatizo hapa ni kwamba katika usajili huu;si kwamba jina la Zanzibar ndiyo lilotumika ila ni jina la Tanzania na hivyo kimataifa jina lote la Tanzania limechafuka.
ReplyDeleteKwa mantiki hiyo inamaana sisi Tanzania bara nasi tumechafuka wakati sisi hata huo usajili hatukuufanya ila Ulifanywa na Zanzibar.
Hizi ndiyo kasoro za Muungano; ifike wakati kila mtu abebe mzigo wake;kama ni kusajili meli za madawa ya kulevya basi kila mtu asajili kwa jina lake mfano Tanganyika au Zanzibar ili ile adha ya kuchafuka jina kama inatokea iwe yako wewe peke yako pasipo kuwachafua na watu wengine wasio husika.Hii ndiyo hoja ya msingi hapa.
Shabani Hamis/mzee wa kugegeda