11 September 2013

MAHABUSU WAFANYA KITUKO MAHAKAMANI



 Na Eliasa Ally, Iringa
MAHABUSU waliofikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa, jana waligoma kuteremka katika karandinga (gari), walilopanda kutoka gerezani ili kuishinikiza mahakama hiyo isikilize kesi zao, kuzitolea uamuzi kwani zimekaa muda mrefu bila kusikilizwa.

Walidai hali hiyo haiwatendei haki kwani wapo baadhi ya watu wanaokamatwa na kuachiwa muda mfupi lakini wao wanaendelea kusota gerezani bila sababu za msingi.Wakizungumza kwa makelele n d an i y a k ar an d in g a h ilo jana, mahabusu hao walisema hawatateremka kwani wengi wao kesi zao zimechukua muda mrefu bila kutolewa hukumu.
"Sisi tunataka haki itendeke, kitendo cha kesi zetu kuchukua zaidi ya miaka minne hadi mitano hakikubaliki, tunaomba kesi zetu zisikilizwe kwa haraka kama zilivyo kesi zingine."Huu ni uonevu wa hali ya juu, tunataka haki itendeke badala ya kuendelea kunyanyaswa na kuonewa kwa kubambikiwa kesi na watu wenye fedha," walilalamika mahabusu hao.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la mahakamani kwa sharti ya kutotajwa majina yao gazetini, walisema mahabusu hao wana madai ya msingi kwani kesi zao zinashindwa kusikilizwa wakiambiwa ushahidi haujakamilika."Tu n a z i omb a ma h a k ama zitende haki kwa kila mshtakiwa, tunashuhudia kesi nyingine zinasikilizwa katika muda mfupi, kwa nini kesi za mahabusu wengine zikwame," walisema.
Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Ramadhan Mungi, alikiri mahabusu hao kugoma kuteremka kwenye karandinga walilokuwa wamepanda kutoka magereza ya mkoa huo."Madai yao ni kesi zao kukaa muda mrefu bila kusikilizwa; hivyo kukaa muda mrefu mahabusu, wengine wanakamatwa na baada ya muda mfupi huachiwa," alisema.
Alisema kutokana na mgomo huo, alimtuma Mkuu wa Upelelezi mkoani humo kwenda kuwasikiliza mahabusu hao na kuzungumza nao ili kuwashawishi wateremke na kwenda kusikiliza kesi zao mahakamani

No comments:

Post a Comment