Na Salim Nyomolelo
KAMPUNI inayohusika na
masuala ya mikopo ya Dun & Bradstreet Credit Bureau imeahidi kuongeza
ufanisi katika utendaji wa shughuli zake baada ya kupokea leseni ya uendeshaji
kutoka Benki Kuu ya Tanzania
(BoT).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Miguel Llenas alisema hatua hiyo
itaiwezesha kampuni yake kutoa huduma za utunzaji wa kumbukumbu za mikopo.
Sambamba na kutoa mikopo kwa ufanisi wa juu na hivyo kuleta
manufaa kwa wateja wake hapa nchini.
" K u t o l e w a k w a l e s e n i kumefungua ukurasa mpya
kwa wadau wote wenye nia ya dhati ya kuona uchumi unaoimarika na wenye nguvu
zaidi. Mfumo huu umeipa sekta ya fedha fursa ya kuboresha huduma za mikopo kwa
urahisi," alisema Llenas.
Alisema, ushirikiano wanaoupata kutoka BoT wakiwemo wadau wengine,
utasaidia mfumo huo wa kumbukumbu za mikopo na wakopaji ulioanzishwa na Benki
Kuu kuleta manufaa makubwa kwa Taifa zaidi katika kukuza uchumi.
"Tunafuraha kubwa kuanza
rasmi uendeshaji wa huduma hii nchini Tanzania, matumaini yetu tutaweza kujenga
na kutoa huduma bora na yenye thamani kwa wadau wote, pia kupitia hatua hii
benki za Tanzania zitaongeza kasi ya huduma zake za mikopo, kupunguza gharama
za uendeshaji na kuwa na taarifa sahihi za utendaji wake," aliongeza
Llenas.
No comments:
Post a Comment