CHAMA cha walemavu wa
ngozi (Albino) nchini kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Taifa
ya Rufaa ya Muhimbili wanatarajia kufanya ukaguzi wa afya kwa jamii ya walemavu
wa ngozi mkoani Tanga katika wilaya tatu za Muheza, Lushoto na Korogwe.Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 22,23 na 24 mwaka
huu katika wilaya hizo
. Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ernest Kimaya alisema hayo
wakati wa kikao cha kujadili changamoto zinazowakabili jamii hiyo katika
upatikanaji wa huduma za afya kilichowahusisha wadau wa sekta ya afya elimu na
huduma nyingine muhimu za kijamii mkoani Tanga.
Kimaya alisema kazi hiyo ambayo wanaamini itawasaidia walemavu wa
ngozi kutambua hali ya afya zao haitakuwa endelevu kutokana na ufinyu wa
bajeti. "Tungetamani sana
kampeni hii iwe endelevu lakini kutokana na ufinyu wa bajeti itabidi ifanyike
katika wilaya chache tu ila tunaomba wafadhili waendelee kujitokeza ili tufikie
watu wengi zaidi," alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo aliiomba Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii kuanzisha kliniki za matibabu ya ngozi katika hospitali na vituo vya
afya nchini kwa ajili ukaguzi wa afya walemavu wa ngozi ili walioathirika na
ugonjwa wa saratani ya ngozi waweze kujitambua mapema. "Unajua tukienda hospitalini watu wanaishia kupewa dawa za
kuzuia mionzi ya jua tu lakini kumbe mwingine tayari ameathirika na saratani
tunaomba kuwe na utaratibu maalum kwa ajili ya walemavu wa ngozi katika vituo
vyote vya afya na hospitali za hapa nchini," alisisitiza Kimaya.
Kuhusu changamoto za ukosefu wa huduma muhimu zinazokosekana
kwa walemavu wa ngozi, Ofisa Ustawi wa Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga,
Eveline Hijja ameziagiza taasisi za afya za Serikali kuwapa kipaumbele walemavu
wa ngozi mara wanapofika katika hospitali na vituo vya afya ili kuepuka dhana
ya unyanyapaa iliyojengeka miongoni mwa jami
No comments:
Post a Comment