27 August 2013

ZITTO: SITAKI URAIS 2015

 • AFICHUA SIRI NZITO KUHUSU UBUNGE WAKE


Na Anneth Kagenda
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), ame s ema h a f i k i r i I kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasiliBw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo

ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam,
Bw. John Mnyika (CHADEMA),"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi...sihitaji urais," alisema.
Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani. Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na
vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na
kupungua kwa mtangamano wa kijamii. Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani
Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fi kra mpya, atakayeleta matumaini mapya,
kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila. Sifa nyingine ni kiongoz mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.
 

9 comments:

 1. Huu ni wakati wa kuzungumzia vipi M4C watawale nchi, Zitto atasaidia kwa kiasi kikubwa chama chake kupiga kampeni nchi nzima za kuichukua ikulu.

  Tunajua mtandao wa makamba kwa watu anaowatumia vyuoni

  ReplyDelete
 2. Pongezi Mh. Zitto kwa kauli yako.

  ReplyDelete
 3. Tatizo kubwa ni waandishi wa habari kuandika yale wanayofikiria wao, mbona kiongozi wa shirikisho la vyuo vikuu kasema kuwa "wanaotoa takwimu za nani anafaa kuwa rais ni wahuni tu na siyo uongozi"

  Hivi kwa haraka tu unaweza kweli kulinganisha zitto na makamba? Makamba ana historia gani ambayo akilinganishwa na zitto apenye? Sasa nadhani urais utakuja kuwa sehemu ya kuvutia bhangi na danguro.

  ReplyDelete
 4. naona mtu anayefaa kuwa rais mwak 2015 si kati ya hao waliotajwa

  ReplyDelete
 5. KWELI KAMA WALIVYOONA WAO MAKAMBA ANAFAA BUT BADO SANA HAJAIVA NA KUKOMAA KIAKILI KULIONGOZA HILI TAIFA AMBAO KWA SASA KUNACHANGAMOTO NYINGI SANA MPAKA KIKWETE ANAZISHINDWA

  ReplyDelete
  Replies
  1. uongozi sio akili wala msomi ila ni busara anazozaliwa nazo. Makamba na Kabwe wana weza sana kuongoza nchi.kwanza wanajua kuchambua mambo kwa haraka na kujenga hoja ya msingi.
   Rais ameshindwa kuamua cha kufanya kwa wakati na anapoamua jambo jema kwa wakati anatanguliza uccm mbele akijua kwamba Taifa kwanza na ccm baadae.
   Huwezi kuwaridhisha wote ila wote wanatakiwa waone umeamua kwa faida ya Taifa.
   aidha kina kabwe na zitto wako wengi sana ila kina kingunge na wasira na komba wanawazibia nafasi. hebu wawape waone nchi itakuwa kwa haraka kinyanja zote

   Delete
  2. Mariki nawewe gombea uraisi. Mbona hupendi wenzako? Hivi unaweza kusimama kiukweli ukasema hao usiowapenda wamekukosea nin?

   Delete
  3. Nchi itakua kwa kisi kiujanja wote!!!! Mariki unafikiri unaendesha Kilimanjaro Express

   Delete