28 August 2013

WATU 27 WAUAWAWA NA FISI GEITANa Daud Magesa, MWANZA
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesema mwaka jana hadi Juni, mwaka huu watu 27 waliuawa na fi si na wanne kujeruhiwa na wanyama hao. Pia fi si 22 wanaodaiwa kujeruhi na kuua watu waliuawa mkoani Geita katika kipindi cha mwaka jana hadi Juni mwaka huu. Kutokana na matukio hayo, 

Wizara hiyo kupitia wataalamu wake, iliamua kutoa elimu kwa wananchi katika vijiji mbalimbali vya Mikoa ya Mwanza na Geita vinavyokabiliwa na changamoto hiyo. Katika mkakati huo vijiji saba vya Senga, Burigi, Katoma, Nyaboge, Sungusira, Igate na Lwenzera vilivyoko mkoani Geita vimenufaika na elimu hiyo ya kujikinga na wanyama hao.
Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo jana na juzi, mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Uenezi Makao Makuu, Twaha Twaibu alisema elimu kama hiyo imetolewa katika vijiji vya Wilaya za Magu na Ilemela mkoani Mwanza. Twaha, alisema familia 93 za waliopata madhara baada ya kujeruhiwa na wanyama wakali wakiwemo fisi walilipwa na Serikali fidia ya sh. Milioni 49,200,000 katika kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa mujibu wa kifungu cha 71 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009.
 Alisema elimu hiyo kwa wananchi inatolewa kwa njia ya mikutano ya hadhara na sinema za kuonesha tabia za wanyama na inalenga kubaini chanzo cha tatizo, ambapo watoto wengi hawamfahamu fi si na wanafananisha na mbwa, kitu ambacho si kweli. Benjamini Kijika, ambaye ni Mkuu wa Kikosi ya ujangili Mwanza na Samweli Nyakonga, Ofisa wanyamapori wa Wilaya ya Geita kwa nyakati tofauti waliwaeleza wananchi wa vijiji hivyo kuwa taarifa zilizopo zinaonesha kuongezeka kwa matukio ya wanyamapori ya kushambulia na kuua binadamu hasa watoto.
Alisema Wizara kwa kuliona tatizo hili imeamua kuwaelimisha wananchi jinsi ya kujikinga na wanyama hao na tabia zao ambao huwinda nyakati za usiku na kuwatahadharisha wananchi wazingatie elimu inayotolewa.Twaha alisema wananchi wanapaswa waone umuhimu wa kuwalinda wanyamapori na mazingira yake hasa wanapokuwa hawaleti madhara,na kuonya vitendo vya ujangili vinavyofanywa na baadhi ya wananchi kuwinda kama swala na wengineo huwakosesha fisi kitoweo na matokeo yake kuvamia mifugo na binadamu chakula mbadala Kuhusu suala la fi si kuhusishwa na ushirikina, Twaha alisema ëJambo hili amelisikia siku nyingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hata hivyo hakuweza kulizungumzia kwani hana ushahidi wa suala hili.Kijika aliwaeleza wananchi wa vijiji hivyo kuwa suala la kusaka fi si limekuwa na vikwazo,yeye kama mtaalamu ameshindwa kuelewa na kuhisi kuna masuala ya ushirikina kuhusu fi si hao.

No comments:

Post a Comment