22 August 2013

YANGA YAPINGA ADHABU YA NGASSA



Na Amina Athumani
UONGOZI wa Yanga leo utawasilisha pingamizi la mchezaji wake, Mrisho Ngasa kutokana na adhabu aliyopewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).Ngassa amefungiwa mechi sita na kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti 17, mwaka huu kati ya Yanga na Mtibwa.Mchezaji huyo amepewa adhabu hiyo, baada ya kubainika kwamba ana mikataba katika Klabu za Simba na Yanga.

 Licha ya kufungiwa mchezaji huyo, pia ametakiwa kuilipa Simba sh. milioni 45 baada ya kuchukua sh. milioni 30 kama sehemu ya mkataba na fidia ya asilimia 50,ambayo ni sh. milioni 15 ambazo Ngassa ametakiwa kuzilipa ndani ya kipindi cha adhabu yake.Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema wanatarajia kuwasilisha mapingamizi matatu TFF kati ya leo na kesho.
A l i s e m a p i n g a m i z i watakalowasilisha kuhusu mchezaji huyo ni kuhusu adhabu aliyopewa, huku barua waliyopewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ikiwa haijaainisha vipengele vya kanuni za kufungiwa kwa mchezaji wao.
"Tulipokea barua kutoka TFF, ambayo inaelezea tu kwamba mchezaji wetu kafungiwa mechi sita na faini ya sh. milioni 45, lakini haijaainisha kipengele chochote cha kanuni za ligi kilichotumika kumuadhibu Ngassa," alisema Mwalusako.Alisema pia ndani ya pingamizi hilo wameelezea kuhusu Simba, kudai kumsajili Ngassa wakati katika barua yao waliwasilisha vielelezo ambavyo si halali.
"Kama ni suala la Ngasa kula pesa za Simba halihusiani na masuala ya usajili lilitakiwa kujadiliwa baina ya Simba, Yanga na mchezaji mwenyewe na si kupelekwa TFF," alisema Mwalusako.Ngasa kabla ya kusajiliwa na Yanga katika msimu uliopita alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo akitokea Azam FC ambayo nayo ilimsajili kutoka kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara

No comments:

Post a Comment