06 August 2013

WATUMIAJI NISHATI,MAJI ZINGATIENI TARATIBU - EWURA CCC


Na Gladness Mboma
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) limewaasa watumiaji wa huduma za nishati na maji kuzingatia taratibu zilizoainishwa katika kanuni inayohusu muda wa kikomo wa kuwasilisha malalamiko ili kusaidia haki kutendeka wakati wa mchakato wa kushughulikia malalamiko husika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa EWURA CCC Mhandisi Profesa Jamidu Katima alisema jana Dar es Salaam kuwa wanalo jukumu la kisheria la kupokea na kusambaza taarifa zinazowahusu watumiaji wa huduma za nishati na maji.
“Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupitia Tangazo la Serikali namba 10, ilichapisha kanuni na taratibu zitakazokuwa zikitumiwa na EWURA katika kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduma za nishati na maji.
“Kwa kuzingatia jukumu hilo, Baraza linawaasa watumiaji wa huduma za nishati na maji kuzingatia taratibu zilizoainishwa katika kanuni hizo, hususan kanuni inayohusu muda kikomo wa kuwasilisha malalamiko EWURA, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia haki kutendeka wakati wa mchakato wa kushughulikia malalamiko husika,” alisema.
Alisema kwenye kanuni ya muda kikomo, kanuni zimeainisha aina sita za malalamiko na kwamba ukiukwaji wa muda kikomo uliowekwa unamaanisha kuwa mlalamikaji atakuwa amepoteza haki yake ya kusikilizwa.
Prof. Katima alisema malalamiko hayo ni pamoja na malalamiko yanayohusiana na kukatiwa huduma bila kufuata utaratibu kupatiwa ankara zisizo sahihi, kushindwa ama kukataliwa kuunganishwa kwenye huduma, kuuza ama kusambaza bidhaa za petroli zisizo na kiwango,kukiuka bei elekezi zilizotolewa na EWURA kwa kuuza ama kusambaza bidhaa za petroli bila kufuata bei iliyoainishwa na EWURA na huduma isiyokidhi kiwango.
“ Wa k a t i m a l a l a m i k o yanayohusiana na kukatiwa huduma bila kufuata utaratibu, kupatiwa ankara zisizo sahihi na kushindwa ama kukataliwa kuunganishwa kwenye huduma yamewekewa muda kikomo wa miezi kumi na mbili kuwasilishwa EWURA, malalamiko ambayo yanahusisha kuuza ama kusambaza bidhaa za petroli zisizo na kiwango yatatakiwa kuwasilishwa EWURA ndani ya siku saba,” alisema.
Alisema muda wa kikomo wa kuwasilisha malalamiko yote yanayohusu uuzaji ama usambazaji wa bidhaa za petroli bila kuzingatia bei elekezi ni miezi sita, wakati muda kikomo wa malalamiko yote yanayohusisha huduma mbovu ni miezi ishirini na minne.
Wakati huo huo, alisema muda kikomo wa kuwasilisha malalamiko ambayo hayapo katika makundi yaliyotajwa hapo juu ni miezi kumi na mbili.
Alisema sababu hasa ya kutoa muda kikomo wa kuwasilisha malalamiko ni kuongeza ufanisi katika kushughulikia matatizo y a w a t u m i a j i wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA kwa kuiwezesha kupata ushahidi utakaoiwezesha kufikia uamuzi wa haki.
“Hivyo basi ni wajibu wa kila mtumiaji wa huduma za nishati na maji kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizowekwa kwenye taratibu za kushughulikia matatizo ya watumiaji ili kuwezesha haki itendeke,” alisema.
Al i s ema EWURA C C C lilianzishwa chini ya sheria ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ya mwaka 2001 ibara ya 414 kifungu cha 30 kwa lengo la kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za nishati na maji.
).

No comments:

Post a Comment