06 August 2013

WANAWAKE 90 WNAOJIUZA KUWEZESHWA,KUPEWA MAFUNZO


SHIRIKA lisilo la Kiserikali la HUHESO Foundation wilayani Kahama mkoani Shinyanga linatarajia kuwawezesha wanawake wapatao 90 wanaoishi katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya UKIMWI kutokana na kujihusisha na biashara ya ngono kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali, anaripoti Patrick Mabula, Kahama
.Akitambulisha mradi huo juzi kwa wadau mjini Kahama Mkurugenzi Mtendaji wa HUHESO, Bw. Juma Mwesigwa alisema jumla ya wanawake 90 wanaojihusisha na biashara ya ngono watapatiwa mafunzo ya ufundi wa ushonaji nguo kwa cherehani.
Bw.Mwe s i gwa a l i s ema HUHESO mradi wake huo una lengo la kuwawezesha wanawake hao kuachana na biashara ya ngono ambapo kati ya hao 90,wanawake 40 watakao pata mafunzo hayo watapatiwa cherehani huku wale 50 watapata mafunzo ya kutengeneza batiki na mishumaa.
Aidha, alisema mafunzo mengine watakayopata ni kutengeneza mafuta ya kujipaka, sabuni, shampoo, mikufu, hereni na bangili, uendeshaji wa biashara ndogondogo na jinsi ya kupata mitaji toka taasisi za fedha lengo ni kuwawezesha kuwa na ajira badala ya kuuza ngono ambayo ni hatari kwa maisha yao.
Bw. Mwesigwa alisema wanawake hao watapatiwa mafunzo hayo kwa miezi sita na kuwa HUHESO tayari imeshaandaa madarasa ikiwa ni pamoja na kuajiri wawezeshaji wa kuwafundisha wenye taaruma hizo wapatao 10.
Alisema wakati wa mafunzo hayo wanawake hao pia watapatiwa elimu ya UKIMWI juu ya athari zake na kujikinga na maambukizi ya VVU katika maisha yao na kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika wilaya ya Kahama.
Kwa upande wao wadau katika mradi huo ambao watakuwa ni viongozi mbalimbali pamoja na watendaji wa kata,maofisa maendeleo ya jamii waliitaka H U H E S O k u h a k i k i s h a inawashirikisha kikamilifu katika kuwateua walengwa bila upendeleo

No comments:

Post a Comment