Derick
Milton, Simiyu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Itilima mkoani Simiyu, kimewataka wale
wote wanaotumia nyumba za ibada, misikiti na makanisa katika kuchochea vurugu
kuacha vitendo hivyo na badala yake waheshimu nyumba hizo ambazo ni maalumu
katika kumuomba Mungu na kumtukuza
.Chama hicho kilisema kuwa hakuna haja ya wanasiasa kila siku kutumia
nyumba za Mungu kueneza chuki ndani ya Watanzania kwani tabia hizo
hazimpendezeshi Mwenyezi Mungu kuhubiri siasa kwenye makanisa na misikiti.
Hayo yalisema jana na Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Itilima
Mohamudu Mabula katika hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na mwenyekiti huyo
katika Ukumbi wa msikiti uliopo mjini Lugulu.
Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kutokukubali baadhi ya watu kuwa
wanatumia nyumba hizo kwa ajili ya kueneza siasa na badala yake kupinga yale
yote yatakayosemwa na watu hao.
Aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kutenda mema katika mwezi Mtukufu
wa Ramadha, huku akiwatahadharisha katika siku za kumaliza mfungo huo
kutojisahau na kuanza kutenda maovu.
"Ni vyema wananchi kuwa na msimamo katika kuhakikisha watu
wanatumia nyumba zetu kueneza siasa pamoja na chuki kuwakataa na kuwapinga
maana wanakuwa hawamtendei mema Mwenyezi Mungu na kitendo hicho ni
kumdhalilisha," alisema Mabula.
Aidha, aliongeza kuwa jamii inatakiwa kuelewa pamoja na wanasiasa kuacha
tabia hizo, na badala yake wajue kuwa msikiti pamoja na makanisa ni nyumba
maalumu kwa ajili ya kumtukuza Mungu pamoja na kuomba mema.
Alieleza kuwa
Watanzania wamekuwa wakijiingiza katika suala la udini, ambapo mwenyekiti huyo
aliwataka Waislamu hao kutokuwa na ubaguzi wa kidini na badala yake waone
Watanzania wa madhehebu mengine kama ndugu zao.
Katika hafla
hiyo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Gorgina Bundala, pamoja
na viongozi wengine wa chama hicho Wilaya, ambapo hafla ya kufuturisha
ilielezwa kuwa ni nguzo kuu moja ya Kiislamu katika mfungo wa Ramadhan.
Mabula aliwataka Waislamu
wote kuwafanya tendo hilo la futuru hasa katika kipindi hiki cha mwisho cha
mfungo wa Ramadhani, akieleza kuwa huu ndiyo wakati maalumu wa kila Mwislamu
kufanya tendo hilo kwa kualika watu mbali mbali kwa madhehebu yote
No comments:
Post a Comment