23 November 2010

Akosa ubunge CHADEMA, atimkia NCCR.

Na Elisante Kitulo.

MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA, Bi. Leticia Mosore ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na chama cha NCCR-MAEGEUZI kwa madai ya kutoridhishwa na
uamuzi wa chama hicho uliomkosesha ubunge wa viti maalumu.

Akitangaza uamuzi huo Dar es Salaam jana, Bi. Mosore alitaja sababu kuu tatu zilifanya afikie uamuzi huo kuwa ni pamoja na udikteta katika kufanya maamuzi, mwenyekiti wa chama kuwa mtia saini na kutoridhishwa na mchakato wa upatikanaji wa wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA.

CHADEMA ililazimika kubadili mfumo wa uchaguzi  wa viti maalumu baada ya kunusa harufu ya rushwa na kumtumia mtalaamu kutoka chuo kikuu kubuni njia mpya, iliyotumia sifa za uzoefu, uwezo wa kuongoza, elimu, uchangiaji wa chama, kuwania ubunge jimboni kutafuta wawakilishi hao.

Kutokana na mfumo huo jina la Bi. Masore halikutokea kati ya majina 25 yaliyoyeuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupata ubunge huo.

Kutokana na kitendo hicho, Bi. Mosore alidai kuwa nafasi hizo zimetolewa kwa kufuata undugu na uhusiano.

"Uchaguzi ni kipimo cha demokrasia si tu kwa serikali bali kwa taasisi zote za kiraia, nikiwa Mwenyekiti wa BAWACHA, sikushirikishwa katika kikao kilichofanya uamuzi wa kuteua majina ya wabunge hao.

Alisema viti maalumu vya sasa vimepatikana baada ya kambi ya Mbowe kuharibu na kuhujumu mchakato halali wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa PTA katika viwanja vya sabasaba.

Alisema akiwa Mwenyekiti wa BAWACHA, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEAMA Taifa (CC), Mjumbe Baraza Kuu la CHADEMA Taifa (NEC) na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani alistahili kuwemo katika orodha ya wabunge 25 wa viti maalumu wa CHADEMA.

"Nilishika nafasi ya tano kwenye matokeo ya uchaguzi wa wanawake wa CHADEMA, lakini leo nimeshindwa kuingia kwenye orodha ya wanawake 25 wa CHADEMA," alihoji.

"Kwa msingi huo sasa, mimi Leticia Ghati Musori, kwa heshima ya utu wangu, na kwa heshima ya wanawake wa CHADEMA Tanzania nzima walioniamini...nimeamua kujiuzulu uenyekiti wa wanawake CHADEMA na kujivua uanachama wa CHADEMA na leo najiunga na NCCR-Mageuzi kutii dhamira na utu wangu," alisema.

5 comments:

  1. TULIYAJUWA NA TULISEMA KUWA MENGI YATAJITOKEZA NA WATAUMBUWANA MMOJA BAADA YA MWINGINE, MAANA UNANYENYEKEWA NA KUHESHIMIKA WAKATI MTU ANATAKA KUKUTUMIA AKISHAPATA HUNA THAMANI TENA!
    NA BADO TUNASUBIRI MVUA MAANA HAYA NI MANYUNYU!
    WALIJINADI KUWA WAMEWATEUA KISOMI NA KWA TAALUMA KUMBE NI CHAGGA DEV' MANFESTO NDIO DIRA

    ReplyDelete
  2. mama yangu siasa ni jambo la kujituma,sasa kama wewe uliingia kwenye chama kwa kutaka cheo bsi utamaliza vyama vyote,na huko ulikoenda sijui kama utadumu,maana hata Mh Mabere Malando kakimbia huko na huyo ndiyo muasisi wa Mageuzi nchini
    haya tunakutakia safari njema kisiasa,maana umetumia demokrasia yako,ila sitashangaa nikisikia uko ccm

    ReplyDelete
  3. Haha!! msimhukumu mtu ambaye anatetea haki yake na wananchi wake kwa ujumla! kwani ukisikia yuko CCM ninicha ajabu kwako? Naona wewe hupendi maendeleo endelea kukandamizwa na hao Chadema ambao dira yao ni chagga development manfesto!!! ambao sio wachaga Chadema siku zao zinahesabiwa upo hapo!!!!

    ReplyDelete
  4. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 23, 2010 at 10:50 AM

    Kati ya hawa yupi ni Mchaga?:Anna Maulida Komu,Leticia Mageni Nyerere,Esther Matiko, Mhonga Luhanywa, Anna Mallac,Paulina Gekul,Conchesta Rwalumulaza, Suzan Kiwanga, Regia Mtema, Christowaja Mtinda,Mwanamrisho Abama , Naomi Kaihula, Christina Lissu,Raya Ibrahim Khamis,Philipa Mturano,Mariam Msabaha,Rachel Mashishanga.Dawa ya unafiki ni takwimu tu.Halafu huyo mama aliyehama,yeye si tayari alikuwa na vyeo mbalimbali? Mbona wenzake hawakuwa na wivu kama wake? Kuvuja kwa pakacha.......

    ReplyDelete
  5. Nathani wewe mama una maslahi binafsi zaidi. Kwa vile umekosa ubunge wa viti maalum ndio unakimbia? Huko NCCR ndio wamefulia kabisa hata uenyeki wa serikali ya mtaa hutapata

    ReplyDelete