01 August 2013

WANANCHI WATILIA SHAKA UTEKELEZAJI ILANI CCM



Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
WAKATI madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakitoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM , wananchi mkoani Morogoro wametangaza kuzitaja kata na majimbo yaliyoshindwa kutekeleza ilani hiyo kwa mujibu wa ahadi walizotoa wakati wakiomba kura kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na wananchi wanachama wa CCM kutoka katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro kutokana na kauli ya Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta kunukuliwa katika vyombo vya habari hivi karibuni uwepo wa wabunge mizigo wanaolala bungeni pasipo kuchangia hoja mbalimbali.
Wanachama hao wa CCM walidai kuwa katika Mkoa wa Morogoro yapo majimbo ambayo wabunge wao wamejisahau kabisa kufanya shughuli walizotumwa na wananchi ambao waliwachagua kuwawakilisha bungeni.
Alisema kuwa utaratibu wa wabunge na madiwani kutoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya CCM uambatane na ahadi walizotoa wakati wakiomba kura kwa wananchi majimboni , badala ya kuishia katika taarifa za vikao vya baraza la madiwani .
Hussein Jumbe mkazi wa jimbo la Mikumi Wilaya ya Kilosa alidai kuwa utaratibu huo wa kutoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya CCM kwa madiwani na wabunge ni vyema taarifa hizo zikawa zinatolewa katika mikutano ya hadhara ili wananchi wapate nafasi ya kuhoji yale yasiyote ndeka.
Naye Fatuma Siwa mkazi wa Jimbo la Kilombero alisema kuwa Mkoa wa Morogoro wabunge wengi wameshindwa kabisa kutekeleza ahadi na ilani hiyo katika kipindi hiki walichokaa madarakani mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment