Na Florah Temba, Rombo
WANAFUNZI 30 kutoka shule mbalimbali za
sekondari katika Wilaya y a Romb o mk o a n i Kilimanjaro walishindwa kuendelea
na masomo katika kipindi cha mwaka 2012 kutokana na kupata ujauzito.Wa n a f u n z
i h a o amb a o walikatisha masomo wengi wao wanaelezewa kuwa walikuwa kidato
cha nne hivyo kujikuta wakitia doa ndoto zao kutokana na kutoendelea na masomo.
Akitoa taarifa
hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake Ofisa Elimu ya Sekondari katika
Wilaya ya Rombo, Juma Kinanda alisema kati ya wanafunzi hao 30 wanafunzi 28 ni
kutoka shule za sekondari za serikali na wawili kutoka shule za binafsi.Kinanda alisema
tatizo la mimba shuleni bado ni tatizo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya
watoto wa kike kukatisha masomo, na hivyo kujikuta wakiishia kuishi maisha ya
mitaani baada ya ndoto zao kuzimika.
Aidha alisema
tatizo hilo limekuwa kubwa na baadhi ya wazazi kutoshtushwa na hali hiyo na
kuona ni jambo la kawaida huku wengine wakidiriki kukataa kutoa ushirikiano
pindi watoto wao wanapobainika kupata ujauzito.
"Tatizo
hili la mimba shuleni liko kwa aina mbili, moja ni wanafunzi wanaopata ujauzito
kugoma kuwataja wahusika ili sheria ichukue mkondo wake kukomesha tatizo,
lakini pili ni wazazi kukataa kutoa ushirikiano kwa wakuu wa shule pindi watoto
wao wanapopata ujauzito, kwa kweli hili ni tatizo ambalo linachangia tatizo
kuendelea kuwa kubwa," alisema Kinanda.
Alisema wapo
baadhi ya wazazi katika Wilaya ya Rombo ambao hudiriki kuwatorosha watoto wao
majumbani kupoteza ushahidi, mara baada ya kugundulika kupata ujauzito wakiwa
shuleni, ili kukwamisha jitihada za wakuu wa shule husika za kufuatilia
wahusika kwa lengo la kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
"Wazazi wamekuwa tatizo kubwa
katika kudhibiti suala hili la mimba mashuleni kwani pamoja na kukataa kutoa
uishirikiano, pia wamekuwa wakiwatorosha watoto wao nyumbani mara baada ya
kugundua kuwa amepata ujauzito na mkuu wa shule anafuatilia ili kumjua muhusika
na kumfikisha katika vyombo vya sheria na hili linawafanya wahusika kuendeleza
vitendo hivyo kutokana na kutochukuliwa hatua zozote," alisema.
Alisema
kukosekana kwa mabweni kumekuwa pia chanzo cha mimba mashuleni kutokana na
kwamba wanafuzni wengi huishi katika nyumba za kupanga (Geto) na hivyo kujikuta
wakijihusisha na masuala ya kimapenzi kutokana na kukosa uangalizi wa wazazi au
walimu.
No comments:
Post a Comment