28 August 2013

WADAU WANOLEWA JINSI YA KUTUMIA KIWANGO CHA ISO Neema Rajab na Flora Nkya (TUDARCO)
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Uledi Musa, amelitaka Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo nchini (SIDO) na kampuni binafsi za biashara kushirikiana na Shirika la Viwango vya Tanzania (TBS) ili kuwahamasisha matumizi ya viwango vya ubora vya kimataifa
.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu huyo, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, wakati akifungua semina ya siku moja iliyoshirikisha wadau mbalimbali kuhusu jinsi ya kutumia kiwango cha Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) 26,000 cha Uwajibika wa Kijamii nchini Tanzania.
Lengo la semina hiyo lililenga kueleza kampuni husika kuwa karibu na jamii wakati zinapotoa maamuzi na kuchukulia umuhimu wa kutunza mazingira, namna ya kufanya kazi na jamii, utii wa sheria bila shuruti ili kuwa na jamii ya Watanzania iliyo endelevu.Alizitaka kampuni na mashirika mbalimbali kujali jamii ambayo ndiyo wanunuzi wakuu wa bidhaa zao na si kujali uzalishaji wao peke yake, japo yote mawili yana mantiki kuongeza mapato.
Aliwaambia washirika wa semina hiyo kuwa zipo faida mbalimbali za wao kushirikiana na TBS na ISO wakati wa uzalishaji wa bidhaa zao, kwani hatua hiyo itawasaidia kutambulika kimataifa na kijipatia soko la bidhaa zao. 
"Ma k amp u n i b i n a f s i n a mashirika ya serikali yanakabiliwa na changamoto ya kufilisika na kushindwa kuendeleza huduma zao kwa jamii kutokana na umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini kwa kushirikiana na TBS na ISO ni rahisi kukabiliana na changamoto hizo kwani lengo ni kuisaidia jamii," alisema Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Viwango wa TBS, Theresia Kessy kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Joseph Masikitiko.
Taasisi ambazo zimeshajiunga kutumia kiwango hicho ni Vodacom Tanzania,Benki ya CRDB, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa upande wake Ofisa Viwango wa TBS,Geofrey Thomas, alisema lengo la semina hiyo ilikuwa ni kueleza kampuni umuhimu wa kuwa karibu na jamii wakati wa kufanya maamuzi. "Watanzania wabadilishe mtazamo kuhusiana na jinsi ya kuhamisha matatizo yanayowazunguka ndani ya jamii na kuyaweka katika biashara yako," alisema.Alisema kiwango hicho namba 26000 kimeanza kutumiwa na makampuni matano nchini na kwamba kwa nchi za Afrika Mashariki kinatumika nchi za Tanzania, Uganda na Kenya.

No comments:

Post a Comment