28 August 2013

UKWEPAJI KODI WACHANGIAARUSHA KUPATA HATI CHAFU



 Na Omari Moyo, Arusha
UKWEPAJI wa kodi unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu katika halmashauri ya jiji la Arusha kunachangia manispaa hiyo kupata hati chafu mara kwa mara.Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema kuwa mianya yote iliyokuwa ikichangia kuingiwa kwa mikataba 'feki' katika miradi ya jiji hilo na ambayo imeiletea jiji hilo hasara kubwa pamoja na ukwepaji kodi itazibwa.

"Nimejichagua mwenyewe kuwa mwenyekiti wa kamati ya mapato ya halmashauri ili kufuatilia kila mahali tunapostahili kulipwa na tumeanza kuona mafanikio; tulikuwa tukipata sh. milioni 400 kwa mwezi; miezi miwili tu iliyopita tumefikia sh. milioni 800 na tunaendelea," alisema Liana.
Aliongeza kwamba, hakutakuwa tena na mikataba ambayo haifuati kanuni wala taratibu na hivyo tenda yoyote na mradi wowote wa halmashauri ya jiji la Arusha haitatolewa kwa kufahamiana wala umaarufu wa mtu wala kupindishwa kwa sheria.
Kutokana na kuongezeka kwa mapato hayo, watajenga mdarasa 39, ya shule za sekondari ili wanafunzi wa mwakani wasikose madarasa ya kusomea pia watanunua magari ya kubebea takataka pamoja na magari makubwa ya ujenzi barabara.Alisema kuwa, yeye madiwani na watendaji wengine wa jiji la Arusha wamejipanga vilivyo kuhakikisha maendeleo katika jiji hilo yanakua kwa kasi ya aina yake.

No comments:

Post a Comment