01 August 2013

VIVUTIO VYA UTALII VYAONGEZEKA VI V U T I O v y a Utalii vinazidi kuongezeka katika visiwa vya Zanzibar baada ya kugunduliwa pango jipya katika eneo la Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja. Pango hilo ambalo linakadiriwa kuwa na urefu wa zaidi ya mita 600 na upana wa mita 25 limegunduliwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho aliyekuwa katika harakati za kumuokoa mnyama katika siku za hivi karibuni
. Baadhi ya wananchi w a l i o z u n g u m z a n a mwandishi wa habari hizi kijijini hapo wamesema wameshatoa taarifa kwa taasisi husika juu ya uwepo wa pango hilo ambalo wanaamini huenda ikawa ni kivutio kwa wageni na kuchangia maendeleo ya kijiji chao na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia kuhusu pango hilo Ofisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dkt. Ussi amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari kwani bado haijafahamika mazingira ya usalama wa pango hadi utakapofanyika utafiti wa kina.
Mapema Kikosi cha Zimamoto na Uokozi walifika katika eneo hilo na kueleza kuwa pango hilo ni refu hivyo kikosi hicho kinafanya tathmini ya masafa ambayo watu wanaweza kufika.
Mkoa wa Kaskazini Unguja ni eneo lenye mapango mengi likiwemo la Mangapwani ambayo yanaelezewa kuwa ni miongoni mwa vivutio vinavyoweza kukuza sekta

No comments:

Post a Comment